Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Kalamu... maneno ya kweli hayo... huu ni mpambano mzito kweli... jamani tuwasaidie mambo mengine tutaendelea kuyafuatilia baadaye.
 
Mwanakijiji.
Vipi bosi wako MBOWE kachangia? na mmekuwa mkisema chadema ni taasisi jee haina uwezo wa kusaidia kwenye matatizo?

Mnyika hutulazimisha tuamini kuwa ni chama mbadala. vipi kwenye matatizo kama haya hakiwezi kuwa chama mbadala?
 
Ndugu zangu suala hili ni lazima lipatiwe ufumbuzi mapema. Nimepewa kadi moja ya ziada na nitaanza kuicheza lakini lazima tuwe na kitu kabla ya ijumaa. What should we do? nataka mawazo....
 
Chuma vijana hata kama wakipewa tiketi hawawezi kurudi! wana deni la kusoma karibu mwaka mzima. Hivi siyo vyuo kama Dar ati unamfukuza mwanafunzi halafu mwanafunzi anakusanya mapakacha na kujirudia kwao. Kwanini wanafikiria vijana wanachotaka ni kurudi nyumbani? Vijana wanataka pesa zao walizotengewa ambao wenzao watatu wameanza kupokea huko huko Ukraine na wengine 12 wanapokea Tanzania (baada ya kukataliwa kuingia Ukraine) zitumwe kwao ili waendelee na masomo. Sasa serikali kutuma tiketi ni kitendo cha kihuni, na kinaonesha hawajalifuatilia jambo hili. Hata hao vijana wakipewa hizo tiketi kuna dalili kesho passport zao zitakamatwa na wao watafikishwa kwa pilato!
 
Sasa mwanakijiji..... hata kama watu watachanga hizo hela je zitajikia hicho kiwango cha wao kumalizia masomo??????? au ni pesa ya wao kuweza kusubiri pesa zao kutoka serikari ya Tanzania ambayo tayari imewakana???????? na kama wanasubiri pesa zao je Serikali itawapatia?????? Serikali ya Tanzania imeshaamua kwamba itawakopesa tiketi ili warudi..... sisi kama watanzania tupo njia panda hatuelewi hatma ya hao wanafunzi ni ipi???????? Wataendelea na masomo huko ukraine????????? na kama wataendelea na masomo je nani atawalipia ada???????? ni michango ya watanzania au serikali amboyo imeshawakana???????? na kama ni Serikari je nani atailazimisha ifanye kitu ambacho mh. President mwenyewe kwa mdomo wake kasema hawatambui na anachoweza kuwasaidia ni Ticket tu!!!!!! tena ni mkopo?
 
Domo Kaya, maswali yako ndiyo kina cha tatizo hili. Tunachojaribu kufanya sasa hivi ni vitu vikubwa vitatu:

a. Kuhakikisha kuwa vijana wanaishi katika maisha ya usalama na wanapata mahali pa kuhifadhi nafsi zao na kupata chakula cha uhakika.

b. Tunajaribu kuhakikisha kuwa deni lao la mwaka mzima linalipwa ili wakitaka kuondoka waondoke na kwenda kokote kule.

c. Tunajaribu kuona kuwa mikopo yao waliyokubaliwa na ikatengwa kwa ajili yao inawafikia licha ya serikali "kuwakana". Kama serikali haitataka kuwadhamini tunafanya juhudi za watu na mashirika binafsi kuwadhamini. Hatuwezi kuacha serikali iamue ni nani anasoma na ni nani asisome. Leo hii kuna wanafunzi wengine wengi tu wanaosoma nje ya nchi je serikali ikikurupuka tu na kusema "haiwatambui" wote tukubali tu kwa vile serikali hadi Rais kasema?

swali lako la mwisho ndio kiini cha usuluhishi wa Tatizo hili. Nani atailazimisha serikali? Ni matumaini yangu watu walioiweka serikali hiyo madarakani. Na hasa wawakilishi wa watu.
 
JK aache unyama. pesa alizokuwa ametenga kwa ajili ya ziara ya real madrid awape hao vijana wakasome.
 
jokakuu,
Unadhani ni nini kati ya ziara ya Madrid na kumsomesha kijana mtanzania kinachoweza kumpa nafasi muungwana kutafutia umaarufu na kula, sorry kura hapo baadae? Hali hii inasikitisha sana.
 
jokakuu,
Unadhani ni nini kati ya ziara ya Madrid na kumsomesha kijana mtanzania kinachoweza kumpa nafasi muungwana kutafutia umaarufu na kula, sorry kura hapo baadae? Hali hii inasikitisha sana.

Sasa hivi Real wamechukua ubingwa watashikika kweli?
 
Mwanakijiji,

You requested for this thread. Here it is... Sorry for a late response nasumbuliwa na mafua hivyo nasinzia sinzia ovyo 🙂
 
Nashukuru... iweke mahali fulani hivi. kwa maana... kuna maendeleo yanayokuja...
 
Marafiki,
Imekuwa ni muda mrefu sana sasa tangu tatizo la wanafunzi liwekwe hadharani. Wanaishije hawa WaTz wenzetu? Jaribu kuwa kwenye nafasi yao, na wingi wa hayo matatizo yanayowakabili! Inauma sana. Hawasomi, wanakula wapi? Wanalala wapi? How do they meet their daily needs? Hii scenario siielewi kabisa! Haieleweki kwa namna yoyote ile bila msaada kutoka nchini Tz. At least people/the government must show some concern na kuchukua matatizo ya wananchi wake kwa uzito fulani. Ni watoto wa waTz maskini. Tafadhali wasaidiwe hata kurudi nyumbani.
 
mie nnatupa malalamiko yangu kwa jf

jamani hawa ndugu zetu wamefikia wapi?

hapa ilikuwa kila thread lazima tukute picha za ndugu zetu hawa, na wengine wakalivalia njuga na kufanya bidii hadi kurusha matangazo na kufikisha habari kila mwahala.

pia tukawa tunaletea hali ya mambo invyoendelea kila siku sio wiki, lkn sasa ni muda hatuna habari yyte.

tuliona mchango ukinadiwa hapa waliobahatika walitoa ila nini kilichoendelea hatukijui.

tuliona petition kunadiwa na kuhimazana tusajili hapa nini kiliendelea hatujui.


vyama vya upinzani nao wakaona ndio pa kutokea kuna mmoja yeye akasema kawapelekea habari yote ya mahojiano na mkuu wa nchi na mwenziwe anaekula ikawa nnasikia yanasikilizwa makao makuu buguruni na kwengineko ila nini kinafuata hatujaeleweshwa tena?

sasa kunani? au ndio tulivyo ? maana hii imewekwa kapuni na sasa tumeingizwa tena uwanjani mwili wa amina ukaguliwe, waje scotland yard, na mengi hili hatujalikamilisha tunaibuka na hili, sasa huu ndio umakini.

wengine tunawaita wasanii jee hawa tuwaiweteje? nnaomba sana nieleweshwe japo ukisema hivi wengine hununa, hupenda kutugeuza wa sesere tuimbe nyimbo wazitakazo wao tu. na kila walionalo wao tuseme hewalwah bwana
 
jamani mbona hapa kimya? vijana wetu vipi weshapatiwa huo msaada au vipi?

serikali iliahidi kuwapelekea chochote warudi nyumbani, wengine wakaona huo ushauri sio mwema, na wakaahidi kulishughulikia tuwape time.

sasa vp mbona kimya au na wao wamekuwa sawa na kina msolla na lowassa au wao wabaya zaidi maana wamewapa matumaini vijana na kuwatupa
 
Back
Top Bottom