Serikali yaweka rekodi kubwa zaidi ya matarajio katika kukuza uchumi

Serikali yaweka rekodi kubwa zaidi ya matarajio katika kukuza uchumi

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Uchumi wa Tanzania umekuwa kwa Asilimia 5.4 tofauti na matarajio ya awali ya Asilimia 4.7 katika robo mwaka ya kwanza ya Mwaka huu wa 2022.

Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kukabiliana na athari za UVIKO-19 na Mgogoro wa Vita ya Urusi na Ukraine umedhihirisha uimara na ukomavu Kwa mujibu wa Takwimu.

Pato ghafi la robo mwaka (Quarterly GDP) imefikia wastani wa TZS Trilioni 34.9 kutoka Trilioni 33.1 Kipindi cha Mwaka 2021.

Kilimo kimechangia 19.6%, jambo hili linatoa tumaini kubwa kwa wakulima kutokana na ruzuku kubwa ya pembejeo katika kilimo inayoendelea kutolewa na serikali.

Juhudi za kukuza italii, uwekezaji, mazingira rafiki ya biashara, mapinduzi katika kilimo, ujenzi wa miundombinu ya kisasa na huduma bora za jamii ni baadhi ya mambo yanayofanywa kwa weledi na Rais Samia Suluhu Hassan.

Watanzania tunazo sababu nyingi za kumpongeza kiongozi wetu huyu makini.
 
Serikali imekosa ubunifu wa kukusanya mapato. Serikali ilitakiwa ibuni vyanzo ambavyo vitamfaidisha mwananchi na yenyewe itanufaika na kodi, sio kuleta kodi zisizo na kichwa wala migui
 
Serikali ilitakiwa ibuni vyanzo ambavyo vitamfaidisha mwananchi na yenyewe itanufaika na kodi, sio kuleta kodi zisizo na kichwa wala migui[/QUOTE]

Upo sahihi sana.

Serikali haitakiwi wakati wote kufikiria namna ya kumnyang'anya kidogo alicho nacho mwananchi bali inatakiwa kuwa bunifu katika kumtengenezea mwananchi mazingira mazuri na rahisi ya kupata pesa zaidi ili na yenyewe ikusanye mapato makubwa zaidi.

Huwezi kuvuna kabla ya kuzalisha.
 
Serikali ilitakiwa ibuni vyanzo ambavyo vitamfaidisha mwananchi na yenyewe itanufaika na kodi, sio kuleta kodi zisizo na kichwa wala migui

Upo sahihi sana.

Serikali haitakiwi wakati wote kufikiria namna ya kumnyang'anya kidogo alicho nacho mwananchi bali inatakiwa kuwa bunifu katika kumtengenezea mwananchi mazingira mazuri na rahisi ya kupata pesa zaidi ili na yenyewe ikusanye mapato makubwa zaidi.

Huwezi kuvuna kabla ya kuzalisha.
[/QUOTE]
Serikali ya Rais Samia Suluhu inalengo la kumuinua mwananchi na sio kumdidimiza ndio maana unaona vijana wanapata mikopo ya masharti nafuu ili waweze kujikwamua kiuchumi pia kupitia miradi inayotekelezwa nchini wananchi wanajipatia ajira kwaiyo kuna vyanzo vingi vya vipato vimeanzishwa
 
Back
Top Bottom