Serikali yazuia wanachama wa NHIF kwenda kuchukua dawa maduka ya nje kwa kufuta matumizi ya form 2c

Serikali yazuia wanachama wa NHIF kwenda kuchukua dawa maduka ya nje kwa kufuta matumizi ya form 2c

Nilimpeleka mgonjwa wangu hospital moja ya rufaa mkoa fulani, Daktari aliandika dawa nikanunua kwenye duka la hospitali husika isipokuwa dawa moja hawakuwa nayo. Hivyo nikaenda kununua duka la nje, nilipofika nilimuomba muhudumu anipigie hesabu zile dawa nilizonunua hospitali, nilishangazwa aliponipa bei yao kuwa ni Tsh. 39,500/= wakati hospitali nilinunua Tsh. 54,000/= . Nikasema sitonunua tena dawa kwenye maduka ya hospitali/serikali.

Sent from my TECNO KD7 using JamiiForums mobile app
Pengine Serikali inauza formulation za Italy, Germany n.k wakati sekta binafsi formulation hizo hizo wanatoa India na Uchina. Kuna tofauti ya ubora......Natania lkn.😅😅
 
Nenda pale MOI Muhimbili ukiandikiwa kuchukua dawa itakuchukua zaidi ya saa 5 kupewa hiyo dawa. Kuna vijana wamewekwa pale ambao wanahangaika na mtandao unakuta anakuambia subiri the network is loading for your service.

Leo serikali inasema inaondoa fomu 2C ikifikiri kuwa wote tuna uwezo wa kumiliki VX za millions of money.

Ummy Mwalimu anaamini matamko na mabarua ya kila cku ndyo utendaji bora wa kazi. Inasikitisha wizara nyeti ya afya za watu inapewa mtu asiyekuwa na ujuzi wa fani husika. Nchi haiwezi kuendeshwa kwa matamko yasiyo na tija toka kwa mawaziri. Ni wkt wa wataalamu kupewa nafasi ya maamuzi kwa ustawi wa sisi sote.
 
Vituo vya afya au hospital zikiishiwa dawa, kuna ubaya gani kununua dawa nje kwenye maduka ili wagonjwa wapone?

Ni nani anapenda kupata usumbufu kutoka hospitali hadi pharmacy kutafuta dawa kama ndani hamna?

Pharmacy za nje zina Watanganyika pia, wanalipa kodi, wameajiri Watanzania na wanatoa huduma ya dawa kuziba upungufu au kuishiwa dawa kwa vituo vya afya/hospitali

Hapa Waziri wa Afya ashauriwe, wasi-handle hili suala too emotional kwenye kutunga kanuni ambayo haiongezi ufanisi kwenye kutoa huduma za dawa na kukosekana dawa kwa wakati kwaweza kugharimu maisha ya wagonjwa.

Kwa anaekumbuka story ya Dr. Isaac Maro wakati anaelezea kifo cha Ephraim Kibonde, ikitokea simply hospital ya Bukoba Mkoani Kagera haikuwa na dawa, mpaka wanagundua dawa hamna ni usiku,na private pharmacy wakawa wamefunga.

Kuchelewa kutoa dawa kwa wakati kwa mgonjwa, kuli-gharimu maisha ya mtu baada ya afya yake kudhoofika.

Weekend njema.

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Pengine Serikali inauza formulation za Italy, Germany n.k wakati sekta binafsi formulation hizo hizo wanatoa India na Uchina. Kuna tofauti ya ubora......Natania lkn.[emoji28][emoji28]
Denk bei zao ni za majuu, wabongo hizo bei hatuzieezi
 
Back
Top Bottom