masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,207
- 13,839
Asante mkuu kwa maoni na mabandiko. Lakini sahihisha .Laiti kama mto Msimbazi ungeboreshwa kwenye njia yake kama ilivyofanyika mto Ng'ombe kuanzia Ubungo, Sinza, Mwananyamala, Manzese na kusishia Mkwajuni Kinondoni ungepumua vizuri. Hata hivyo barabara kutokea Magomeni Morocco hoteli kwenda Kinondoni kupitia Mkwajuni iko chini sana mvua zikinyesha maji yapita juu yake kiasi cha kusababisha usumbufu kwa watumiaji.
Shida ya mto Msimbazi inaanza baada ya kupita Segerea kuelekea baharini, watu wamejenga kando ya mto na kuendesha shughuli za kibinadamu pembeni mwake kiasi cha kufanya ukinzani wa mkondo wa maji. Hapo mpaka kuna viwanda vilivyopewa vibali na serikali wakajenga kukinzana na mkondo wa maji kuanzia maeneo ya bonde la Kigogo shuka mpaka bonde la Magomeni mzimuni watu wamejenga mpaka kwenye kingo za mto huko serikali ipo, vibanda vingi vilivyoondolewa Kariakoo vya vifaa vilivyotumika pamoja na kituo cha malori ya kukodi usafirishaji mizigo kwenda mikoani vimehamishiwa kwenye bonde la jangwani.
Bonde la jangwani awamu ya tano lilianza kunawiri kwa uoto wa asili lakini awamu hii ilipoingia watu wamevamiwa na kuanzisha shughuli za kibinadmu kama kilimo, kukata miti na kurudi kinyemela kwa raia waliohamishwa kwenye nyumbani zinazoambaa kuelekea ofosi za Yanga.
Ujenzi wa barabara kuanzia Magomeni mataa kwenye 'Fire' haukuzingatia taaluma ya uhandisi ila siasa ndio zilitawala kuonesha wananchi wamejengewa miundo mbinu imara bila ya kufkiri endapo mvua kubwa hasa kutokea Kisarawe ingenyesha madhara gani yangetokea kwenye bonde hilo. Halafu bila kujali kituo kikuu cha mabasi ya mwendo kasi kikajengwa sambamba na na kingo za mto ambazo hutumika kupumua pindi maji yakijaa.
Sehemu lilipojengwa daraja la Selander ni ingilio la mto Msimbazi baharini lakini pia nia 'vent' ya kupumulia bahari. Kuna daraja mbili
1. Moja ni nyembamba ambayo sana sana kwa sasa wanatumia watembea kwa miguu kupita upande wa kusini magharibi mkabala na msitu wa miti ya mikoko, lilijengwa na wakoloni kwa matumizi ya wazungu kati ya mwaka 1920-1949
2. Pili ni daraja linaloenda sambamba na lile finyu ambalo kwa sasa ndio linatumika kupitia magari lilijengwa na Tanzania miaka ya 1972 hivi ambalo lilipata umaarufu sana pale mwana mziki mmoja wa Tanzania alipoimba wimbo wa 'Zuwena' aliimba Marijani Rajab.
Maingilio ya mto Msimbazi na bahari kwenye daraja la Salender na miti ya mikoko ni hatarishi sana tangu makaburu walipue daraja la kwanza imekuwa ni maficho na mvizio wa waharifu wengi kupora raia hata mauaji miili hukotwa ikiwa imetupwa chini ya daraja au kwenye mikoko. Hata Hamza alipora bunduki kuanzia eneo lilio karibu na salender kuelekea ubalozi wa Ufaransa akishambulia askari polisi. Hata ubalozi wa Marekani uliolipuliwa mwaka 1998 ulikuwa karibu na eneo hilo kabla ya kuhamia Msasani Drive Inn.
USHAURI
1. Raia wote wanaoishi pembeni ya mto Msimbazi kuanzia Kigogo mpaka Magomeni, Jangwani, Mkwajuni, Kinondoni shamba na karibu na Muhimbili waondoshwe maana walifidiwa na kupewa viwanja Mabwepande 2013-2015
2. Lijengwe daraja la juu kuanzia Magomeni mapipa hadi 'Fire' Kariakoo
3. Kituo cha malori ya kukodi, nyumba za kuishi na vibanda kutokea ofisi za Yanga hadi mzunguko wa Kigogo ziondoshwe
4. Lijengwe daraja la juu kuanzia Morocco hoteli, Magomeni hadi Mkwajuni Kinondoni kuepuka usumbufu wa mafuriko
5. Bonde linalobaki chini lioteshwe miti kutunza mazingira na kusaidia uchujaji wa hewa iliyochafuliwa kutokana na uchafu wa moshi, harufu mbaya za vitu vilivyooza au kemikli za viwandani
6. Katika bonde hilo litengwe eneo liboreshwe kwa mapumziko 'Recreational Park'
7. Shughuli za kilimo zipigwe marufuku na sheria itungwe kulinda ukiukwaji unaofanywa na binadamu kwa makusudi
8. Kituo cha polisi Salendar kiboreshwe zaidi na vifaa vya usalama vifungwe kuzunguka daraja ili kusaidia kubaini uharifu mapema
9. Msitu wa mikoko na daraja la Salender vihifadhiwe vyema na kupewa hadhi ya eneo la kiutalii (The Silent War: South African Recce Operations 1969-1994 by Peter Stiff)
TANBIHI: Kitu gani kilikwamisha utekelezaji wa mradi huu ulioanzishwa 2018-2020?
Reference:
Mafuriko Msimbazi Dar: Mwarobaini watua Ofisi ya Rais
Usuli Kwa mujibu wa Kanzidata ya Kimataifa kuhusu Majanga Asilia yaliyotokea tangu mwaka 1990, Tanzania inakabiliwa na hatari ya majanga asilia yafuatayo, frikwensi zake zikiwa zimeonyeshwa katika mabano: mafuriko (62.2%), ukame (13.3%), tetemeko la ardhi (11.1%), kimbunga (8.9%), moto wa...www.jamiiforums.com
![]()
The Msimbazi Opportunity : Transforming the Msimbazi Basin into a Beacon of Urban Resilience (Vol. 2) : Volume A - Strategy and Management Framework
Responding to the call of Vice President of Tanzania, Honourable Samia Suluhu Hassan, to pragmatically address the recurrent flood risk in Dar es Salaam, the Msimbazi .documents.worldbank.org
![]()
Transforming Tanzania’s Msimbazi River from a Liability into an Opportunity
A consultative process brought together stakeholders to generate a new blueprint that will turn a key river from a hazardous liability into a beacon of urban resiliencewww.worldbank.org
Selander Bridge original ( lile la zamani) lilijengwa mwaka 1929, hili ndilo karibu litabomoka kama tunavyoona kwenye picha.
Na maboresho yake yalijengwa na serikali ya Japan kupitia shirika lake la misaada, JICA mwaka 1980.
Siyo 1972 kama ulivyo andika.