BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Huku mtaani kwetu kuna shule nyingi ambazo hazina uzio na mazingira yake pembeni yamekuwa na mitimiti ambayo ikifika mida ya jioni kunakuwa na mazingira flani ambayo ni hatarishi kwa wanafunzi.
Sisi wenyewe ndio tumesoma kwenye shule nyingi za aina hiyo lakini sasa hivi tumekuwa nimegundua kuwa tulikuwa katika mazingira flani hatarishi kinoma
Ukifatilia sasa hivi mitaani kuna michongo mingi ya matukio ya ukatili kwa watoto na wanawake, sasa mazingira kama hayo ya mitimiti na vichaka ni hatarishi sana kwa wadogo zetu walipo shuleni.
Nashauri serikali kupitia ngazi za mtaani kama walivyofanya kampeni ya kuongeza madawati, wafanye hivyo pia katika kuboresha usalama kwenye shule za kila mtaa hasa zile ambazo hazina uzio na kuna vichaka jirani na shuleni.
Hivi vichaka siyo vya kuamini kabisa, matukio mengi ya ajabu yanatokea, hatua zichukuliwe
Kukosekana kwa uzio pamoja na wanafunzi kutembea umbali mrefu katika maeneo yanayozungukwa na vichaka wakati wa kutoka nyumbani kwenda shule zimetajwa kuwa changamoto kubwa zinazohatarisha kuongezeka kwa matukio ya ukatili.