Serikalini watu tunaishi kwa kuiba; huu ndo ukweli

Serikalini watu tunaishi kwa kuiba; huu ndo ukweli

Tanzania bila wizi inawezekana , nyie ndio mnafuga na kuwapa sapoti wezi kwa kuwafariji.
Inawezekana kama serikali itakua inajali maslahi ya wafanya kazi Maana watu wanapigwa spana kwenye mshahara bado wakija kustafu bado wanakutana na kikokotoo cha wastafu 🤣🤣🤣acha waibe
 
Majizi yako humu yameuchuna tu tena mengine yatajifanya kukemea tabia ya wizi.

Ngoja niwambie ukweli .Serikali haina shukrani itakutumia kama kondomu ukuisha muda inakudampo. Tena unaweza kufanya mazuri mia moja ila kosa moja tu itakuadabisha. Kwahiyo jamani wewe ukijifanya mzalendo itafika muda wako wa kustafu utatoka na uzalendo wako.

Muhimu ni kwamba ukipata upenyo wa kupiga we piga tumia amri ya kumi na sita ya shetani inayosema "Usihurumie kiumbe ambacho haukukiumba".
Makanisani viongozi wanapiga sembuse serikalini.
Wewe jifanye mzalendo utakufa masikini na uzalendo wako.
Ona Sasa! Yaani raia wa nchi hii wameharibika hivi! Kumbuka cha kuiba kina laana
 
Bila wizi hii mishahara tusingeweza kufanya jambo lolote

Ndo maana walimu wanalia Sana ni kwa sababu hawana sehemu ya kuokota .

Hakuna MTU ambaye haibi wala kupiga dili .
Kuiba mda we unaona ni jambo dogo ?
Mtu anapiga kipindi halafu anapotea mazima mpaka tu moro.
Kabla ya Magu kuna walimu waliiba mda wa serikali kufuru ! Astaghafirulah toba !
Tema mate chini dogo, ni vile kamera hazipo mashuleni. Unakuta mtu ijumaa hajawahi gusa chaki yupo kuleeeeeeeee!
 
Unaihalalisha wizi sio!!

Wizi husababisha MAUTI, pesa ya wizi ukianzishia biashara lazima biashara ife, sababu mtaji haukutokana na source halali.

Na jela ya kusubiri.
 
Uko sahihi jamaa,imagine traffic wafanye haki wasichukue hela yoyote ya kiwi wategemee salary?
Daktari usiwe na dili la hospital jirani au binafsi(kuiba muda wa muajiri)utegemee salary,we hakuna kutoboa
 
Back
Top Bottom