Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija

Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Naangalia kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari kinachorushwa na Star TV, ambapo mwandishi Mkongwe, Deo Masakilija, amealikwa.

Dotto Bulendu ameanza kwa hoja 'Je media imetimiza wajibu wake ipasavyo katika kuwabaini hawa watu wasiojulikana wanaohusika na matukio ya utekaji, utesaji, uvamizi, mashambulizi ya silaha na mauaji ya Kibiti ambapo vitendo vyote hivyo, vimefanywa na watu wasiojulikana, media imeshindwa nini kuisaidia jamii kuwabaini hawa wasiojulikana?'.

Deo Masakilija anasema media inaweza kuwabaini hawa watu wasiojulikana kwa media kuwatumia waandishi mahiri wa IJ, (Investigative Journalism), hatua ya kwanza ni kwa media ku invest kwenye kutafuta ukweli kwanza kwa kujenga uwezo wa IJ skills kwa waandishi wake(capacity building), kisha hiyo media kuwawezesha waandishi wake kufanya IJ.

Masakilija anasema kama mauaji ya Kibiti, serious media ingetuma IJ Kibiti na kupiga kambi Kibiti na kufanya urafiki na watu in friendly manner, lazima wananchi wangejitolea kutoa ushirikiano.

Bulendu akauliza kwenye tukio la kushambuliwa kwa Tundu Lissu, kwanini media haikwenda kwenye eneo la tukio kupata independent witnesses report ya mashuhuda?.

Kwanini media haikwenda Dodoma Hospital kupata taarifa ya kidakitari Lissu alivyojeruhiwa?

Kwanini media haikumhoji shahidi mkuu dereva wa Lissu pale Dodoma ili kupata kilichotokea na tukio zima lilivyokuwa?

Kwanini mpaka sasa hakuna media iliyotuma mtu Nairobi kupata maendeleo ya Lissu na kumhoji dereva wa Lissu?

Kama kuliwahi kutokea mashambulizi na mauaji ya aina, media imeshindwaje to connect the dots.

Hitimisho:
Kwenye hili tukio la kushambuliwa kwa Tundu Lissu, Tanzania tumeonyesha hatuna kabisa serious media kufanya IJ, hivyo media haijatimiza wajibu wake.

Paskali
Rejea
Waandishi wa habari wa Tanzania, wamekuwa waoga kupitiliza kisa kuambiwa UCHOCHEZI

Werema: Hatuna waandishi wa habari za uchunguzi Tanzania bali wahemea kodi za pango

Stan Katabalo: Tunauhitaji mzimu wako wa habari za Uchunguzi!
 
labda wawe waandishi waliofunzwa mambo yakijasusi hivihivi kuna vitu vitakuwa vinawapita ktk uchunguzi wao pia watakuwa kwenye hatari ya kuuliwa,waanze kuandamana kupigwa mabomu ya machozi mpk basi kazi bure!.. mambo kama hayo yanahitaji ujasiri si hovyohovyo maana unajikuta unacheza na watu wakubwa ukishatoa taarifa zao usalama wako uko wapi..?
kama wabunge wanatendewa hivyo itakuwaje kwa waandishi...
 
asilimia 95% ya waandishi wa habari hawana sifa stahiki ktk taaruma yao imekua vigumu kutambua mipaka yao ya kazi
 
Nilikuwa Namsikiliza Vizuri Yohana Gwangay Ndyo Ameulezea Vizuri,inawezekana Kabisa Kwakuanzia Kwnye Eneo La Tukio Nakuendelea Na Source Nyngne
 
Wewe mwenyewe unaonekana haupo serious investigative journalism haichukui siku moja.
Mkuu Buria, kwanza bandiko hili ni la reporting kinachozungumzwa Mwanza, where Do I come along?. Pili kuna mahali nimesema IJ ni siku moja?. Niliposema Kibiti Media zitume IJ kupiga kambi Kibiti, nilimanisha nini?. Au kambi ya siku moja?.
 
Kipindi kimemalizika
P
Kipindi cha leo kimekuwa kizuri kama vile ambavyo Dotto alikuwa anawaalikeni nyie. Hata katikati alianza kupotoka kwa kualika watetezi sio wa hoja bali hoja za nguvu wa serikali na misimamo ya chama.
Suala la Investigative Journalist ni muhimu sana katika kujenga uwezo wa kuweka mambo mengi wazi kuliko kutegemea zile Press za ma RPC na kuandika kasema nini. Suala la wale wafanya biashara wa Kilosa kama sio waandishi wachunguzi lisingefikia mahali haki ikapatikana kwani press za Polisi zilisema hao ni majambazi na wameuawa wakijibishana kwa risasi na polisi. Hebu ona uongo huo kutoka katika chombo tunachoambiwa tukiamini.
Tatizo waandishi wengi habari za kiuchunguzi hawajiwezi, na nimeona hakuna juhudi zozote za kuwasaidia waandishi wachanga kuongeza ujuzi. Kidogo sana UTPC wamekuwa wanaandaa mafunzo kupitia Klabu za waandishi za mikoa mara kwa mara lakini vyombo kama MCT hawana habari kabisa. Na mbaya zaidi ni kuwa Klabu hizo hata waandishi wenyewe hawazithamini, unaweza kukuta hata wewe Pasco sio mwanachama wa Dar Press Club au sio mwanachama hai. Nenda Mwanza nako waweza kukuta Dotto naye sio mwanachama wa Mwanza Press Club au sio mwanachama hai. Nani atawasimamia mfanyapo kazi ya hatari kama habari za kiuchunguzi (IJ)?
Waandishi wajifunze kujijengea nguvu zao kwa kuhakikisha vyama vyao (vya waandishi) vinakuwa na nguvu kama TLS na kamwe wasidhani vitu kama MOAT au lile jukwaa la wahariri ni vyombo vyao.
Bila kuwekeza katika kujifunza habari za kiuchunguzi (IJ) tasinia ya habari hapa nchini itazidi kudharaulika na kuonekana ni tasnia ya bahasha tuu.
 
Shemeji Pascal pole japo wanasema mjumbe hauawi naona jinsi ulivyopondwa mawe pole sana.

Hivi kuna hata media moja ilimuuliza mwanampendwa wa Mfalme alikuwa wapi siku ya tukio??Maswali matatu magumu yangemchanganya angesema ukweli uliokaribu na tukio??

Kuna aliyemuuliza Morogoro alifuata nini asubuhi kuchwe wanafanya mazoezi saa 11 asubuhi ilikuwaje??

Mbona hakuwepo kwenye kuvunja Report ya Makinikia ya Almasi pale Ikulu??

Hivi siku ya tukio alienda kuuza sura wapi maana Mtoto wa Mfalme anapenda kupugwa picha sana tu.

Hivi wale walinzi wakishaulizwa kwamba ilikuwaje??Au RPC Dodoma ameshaulizwa au kuwa interviewed kwamba kwani I washika SMG pale getini kwa makubwa hawakuwepo wala hawakusogea kwenye tukio??Au sababu aliyekuwa anamiminiwa zile.risasi ni Jambazi
 
Back
Top Bottom