Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija

Shemeji Pascal pole japo wanasema mjumbe hauawi naona jinsi ulivyopondwa mawe pole sana.

Hivi kuna hata media moja ilimuuliza mwanampendwa wa Mfalme alikuwa wapi siku ya tukio??Maswali matatu magumu yangemchanganya angesema ukweli uliokaribu na tukio??

Kuna aliyemuuliza Morogoro alifuata nini asubuhi kuchwe wanafanya mazoezi saa 11 asubuhi ilikuwaje??

Mbona hakuwepo kwenye kuvunja Report ya Makinikia ya Almasi pale Ikulu??

Hivi siku ya tukio alienda kuuza sura wapi maana Mtoto wa Mfalme anapenda kupugwa picha sana tu.

Hivi wale walinzi wakishaulizwa kwamba ilikuwaje??Au RPC Dodoma ameshaulizwa au kuwa interviewed kwamba kwani I washika SMG pale getini kwa makubwa hawakuwepo wala hawakusogea kwenye tukio??Au sababu aliyekuwa anamiminiwa zile.risasi ni Jambazi
amepigwa risasi rais wa Marekani John F. Kenedy na kuuwawa ije kuwa Tundu Lisu
 
Sekta ya uandishi wa habari Tanzania bado ni changa sana. Kuna vijana wengi tu ktk hizi FM radios-hasa za mikoani ambao malipo yao ni kusikika redioni! Hakuna cha mshahara wala posho, kazi ni kwako kutumia kujulikana kwako kujipatia kipato. Jirani tu hapo Kenya, Janeth Mbugua alikuwa anakamata milioni 20 kwa mwezi wakati yupo The Citizen TV na kazi yake kuu ilikuwa kusoma habari tu!

Kuna wakati tulikuwa na Jerry Muro, ila rushwa ikampenda zaidi. Toka hapo hakuna anayetamani kuvaa viatu vya Stan Katabalo.
 
Ukijiuliza haya maswali:

1. Dereva wa Lissu ni mtu wa miraba 4, hivyo kwa kumuangalia alikuwa dereva cam mlinzi, lakini hakuguswa hata risasi 1 kati ya hizo nyingi zilizofyatuliwa, alikuwa kajificha wapi ambapo hapakulengwa na kwa nini kusilengwe na washambuliaji?

2. Lakini kitendo tu cha kwenda naye Nairobi kwa kisingizio chechote kile, khalafu gharama za matibabu zinaongelewa za Lissu hakuna anayetaka kutaja neno shoferi basi jua media iko na nguvu kubwa za kiuchunguzi na hilo linajulikana. Pole hizi zimfikie Mh Lissu hapo hospitalini Narobi.

Mchina wa hF.
Na washawasha!
 
Wanabodi,

Naangalia kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari kinachorushwa na Star TV, ambapo mwandishi Mkongwe, Deo Masakilija, amealikwa.

Dotto Bulendu ameanza kwa hoja 'Je media imetimiza wajibu wake ipasavyo katika kuwabaini hawa watu wasiojulikana wanaohusika na matukio ya utekaji, utesaji, uvamizi, mashambulizi ya silaha na mauaji ya Kibiti ambapo vitendo vyote hivyo, vimefanywa na watu wasiojulikana, media imeshindwa nini kuisaidia jamii kuwabaini hawa wasiojulikana?'.

Deo Masakilija anasema media inaweza kuwabaini hawa watu wasiojulikana kwa media kuwatumia waandishi mahiri wa IJ, (Investigative Journalism), hatua ya kwanza ni kwa media ku invest kwenye kutafuta ukweli kwanza kwa kujenga uwezo wa IJ skills kwa waandishi wake(capacity building), kisha hiyo media kuwawezesha waandishi wake kufanya IJ.

Masakilija anasema kama mauaji ya Kibiti, serious media ingetuma IJ Kibiti na kupiga kambi Kibiti na kufanya urafiki na watu in friendly manner, lazima wananchi wangejitolea kutoa ushirikiano.

Bulendu akauliza kwenye tukio la kushambuliwa kwa Tundu Lissu, kwanini media haikwenda kwenye eneo la tukio kupata independent witnesses report ya mashuhuda?.

Kwanini media haikwenda Dodoma Hospital kupata taarifa ya kidakitari Lissu alivyojeruhiwa?

Kwanini media haikumhoji shahidi mkuu dereva wa Lissu pale Dodoma ili kupata kilichotokea na tukio zima lilivyokuwa?

Kwanini mpaka sasa hakuna media iliyotuma mtu Nairobi kupata maendeleo ya Lissu na kumhoji dereva wa Lissu?

Kama kuliwahi kutokea mashambulizi na mauaji ya aina, media imeshindwaje to connect the dots.

Hitimisho:
Kwenye hili tukio la kushambuliwa kwa Tundu Lissu, Tanzania tumeonyesha hatuna kabisa serious media kufanya IJ, hivyo media haijatimiza wajibu wake.

Paskali
Rejea
Waandishi wa habari wa Tanzania, wamekuwa waoga kupitiliza kisa kuambiwa UCHOCHEZI

Werema: Hatuna waandishi wa habari za uchunguzi Tanzania bali wahemea kodi za pango

Stan Katabalo: Tunauhitaji mzimu wako wa habari za Uchunguzi!
Hili la lissu halihitaji uchunguzi kwani tiyari wanajulikana kuwa ni wasukama kadhaa ila hakuna mwenye ubavu, guts, kuwaaanika hadharani
 
Waandishi wapo na wanaweza kufanya kazi nzuri, ishu moja ambayo ndio ishakuwa kubwa waandishi wameeacha kutetea tasnia yao katika uandishi wa habari. Wanasiasa wamewaingilia, serikali imewaingilia hawana pa kupumulia
 
Sekta ya uandishi wa habari Tanzania bado ni changa sana. Kuna vijana wengi tu ktk hizi FM radios-hasa za mikoani ambao malipo yao ni kusikika redioni! Hakuna cha mshahara wala posho, kazi ni kwako kutumia kujulikana kwako kujipatia kipato. Jirani tu hapo Kenya, Janeth Mbugua alikuwa anakamata milioni 20 kwa mwezi wakati yupo The Citizen TV na kazi yake kuu ilikuwa kusoma habari tu!

Kuna wakati tulikuwa na Jerry Muro, ila rushwa ikampenda zaidi. Toka hapo hakuna anayetamani kuvaa viatu vya Stan Katabalo.
Kituo cha Television cha KTN kupitia kipindi chake cha Jicho Pevu limefanya kazi nzuri sana kwasababu waandishi walilipwa vizuri na kupewa vitendea kazi angalia clip kuhusu Kifo cha Saitoti.
 
Kama waandishi wenyewe ndio wale walipewa fursa ya kumwuliza maswali mtukufu rais halafu eti anauliza " ni kitu gani kigeni umekiona ikulu" mwingine eti " mh. unapendelea kitu gani"
Hapo unategemea nini?
 
Wanabodi,

Naangalia kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari kinachorushwa na Star TV, ambapo mwandishi Mkongwe, Deo Masakilija, amealikwa.

Dotto Bulendu ameanza kwa hoja 'Je media imetimiza wajibu wake ipasavyo katika kuwabaini hawa watu wasiojulikana wanaohusika na matukio ya utekaji, utesaji, uvamizi, mashambulizi ya silaha na mauaji ya Kibiti ambapo vitendo vyote hivyo, vimefanywa na watu wasiojulikana, media imeshindwa nini kuisaidia jamii kuwabaini hawa wasiojulikana?'.

Deo Masakilija anasema media inaweza kuwabaini hawa watu wasiojulikana kwa media kuwatumia waandishi mahiri wa IJ, (Investigative Journalism), hatua ya kwanza ni kwa media ku invest kwenye kutafuta ukweli kwanza kwa kujenga uwezo wa IJ skills kwa waandishi wake(capacity building), kisha hiyo media kuwawezesha waandishi wake kufanya IJ.

Masakilija anasema kama mauaji ya Kibiti, serious media ingetuma IJ Kibiti na kupiga kambi Kibiti na kufanya urafiki na watu in friendly manner, lazima wananchi wangejitolea kutoa ushirikiano.

Bulendu akauliza kwenye tukio la kushambuliwa kwa Tundu Lissu, kwanini media haikwenda kwenye eneo la tukio kupata independent witnesses report ya mashuhuda?.

Kwanini media haikwenda Dodoma Hospital kupata taarifa ya kidakitari Lissu alivyojeruhiwa?

Kwanini media haikumhoji shahidi mkuu dereva wa Lissu pale Dodoma ili kupata kilichotokea na tukio zima lilivyokuwa?

Kwanini mpaka sasa hakuna media iliyotuma mtu Nairobi kupata maendeleo ya Lissu na kumhoji dereva wa Lissu?

Kama kuliwahi kutokea mashambulizi na mauaji ya aina, media imeshindwaje to connect the dots.

Hitimisho:
Kwenye hili tukio la kushambuliwa kwa Tundu Lissu, Tanzania tumeonyesha hatuna kabisa serious media kufanya IJ, hivyo media haijatimiza wajibu wake.

Paskali
Rejea
Waandishi wa habari wa Tanzania, wamekuwa waoga kupitiliza kisa kuambiwa UCHOCHEZI

Werema: Hatuna waandishi wa habari za uchunguzi Tanzania bali wahemea kodi za pango

Stan Katabalo: Tunauhitaji mzimu wako wa habari za Uchunguzi!
Yes ''Investigative Journalism'' Do they have power to interrogate and summon, Suppose the Authority turn on a deaf ear What can investigate journalism do
 
Paskali
Ukifanya serious IJ nchi hii yafuatayo yatakufika
1) Dr Abbas atafungia chombo chako
2) Utapimwa mkojo
3)Utaburutwa mahakamani kwa uchochezi
4) Watu wasiojulikana' watakufanyia kama Kibanda na Kubenea

Utawalaumu waandishi kwa woga?
 
Back
Top Bottom