Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija

Mkuu Paskal iwapo utafanya IJ yatakukuta yaliyomkuta Lissu. Toka imeingia awamu hii ni nani alibaki anaweka mapungufu ya awamu hii kwa uwazi zaidi ya Tindu Lissu? Uliwahi kusikia muandishi yoyote aliyehoji kwanini ndege haifiki? Kwa sasa ili kuweza kufanya IJ inabidi kujitoa muhanga kama Lissu. Kinyume na hapo watu wangoje taarifa toka kwa polisi wenye weledi mdogo.
 
Ili mtume pandikizi kama Okoth..
.hakuna mtakalo waza hatuja waza
 
Waandishi wakibongo wanaenda kwenye Pres.. wakiwa wamevaa Vizibao vyenye Logo ya Chama cha SIASA wanavizia teuzi unategemea nini... Mtu kama Mohamed Ally wa KENYA muda huu wasiojulikana tungeshawajua... na mtu mwingine alikuwa kUBENEA
tangu alipomwagiwa Tindikali GAZETI lake limeishia kuandika uLALAMISHI
 
Paskali
Ukifanya serious IJ nchi hii yafuatayo yatakufika
1) Dr Abbas atafungia chombo chako
2) Utapimwa mkojo
3)Utaburutwa mahakamani kwa uchochezi
4) Watu wasiojulikana' watakufanyia kama Kibanda na Kubenea


Utawalaumu waandishi kwa woga?
Kwa uharamia naamini KENYA bado hatujawafikia
natamani kujua Kwanini Mohamed Ally anafanikiwa kwenye Mission zake... kwa mtazamo wangu
Waandishi wetu hawapandi hiyo Kazi ya Uandishi wanafanya kwaajili ya kuganga Njaa...ndio maana wanajipendekeza kwa watawala ili wateuliwe kwenye uDC
Nk
 
Mkuu Buria, kwanza bandiko hili ni la reporting kinachozungumzwa Mwanza, where Do I come along?. Pili kuna mahali nimesema IJ ni siku moja?. Niliposema Kibiti Media zitume IJ kupiga kambi Kibiti, nilimanisha nini?. Au kambi ya siku moja?.
Utulie kwa sababu Bwana Mayalla(Njaaa)!bado I Journalists tusiojulikana tupo kazini kimya kimya.Nyinyi "Tender-Journalists" hili hamliwezi.Vp tender bado zinatoka mwaka wenu huu Mr Njaa
 
Mkuu Paskali,
Mi nadhani watu 'WASIOJULIKANA' hatujaanza nao leo... walikuwepo na wapo toka kitambo... SI MEDIA pekee ya kulaumiwa kwenye hili...

Tuna hurka ya 'KUWA NA WATU WASIOJULIKANA' kwenye mambo yaliyo na mslahi kitaifa
1. Wale wa EPA ambao walirudisha kile tulichopigwa, NI WATU WASIOJULIKANA
2. Tume mbalimbali zimekuwa zikiundwa, lakini ndani yake kuna watu wasiojulika
3. Waziri mkuu mstaafu, mh. Pinda, hakutaja wale wa meremeta kwamba nchi ingetikisika... WATU WASIOJULIKANA WANGETIKISA NCHI
4. Juzi tu hapa, tume ya almasi imesema MTU MMOJA ASIYEJULIKANA ALIPEWA ALMASI YA MAMILIONI YA PESA
5. WATU WASIOJULIKANA walishughurika na Mwakyembe
6. WATU WASIOJULIKANA wameshughurika na ROMA MKATOLIKI

Kwa hiyo si media tu...
Ngali K
 
Kwa vile neno "media" kwa sasa linajumuisha pia mitandao ya kijamii kama vile blogu, basi naomba japo kidogo nisikubali lawama hizo kwa "media" zetu.

Baadhi yetu (mabloga) twajaribu, na baadhi ya mifano hai nii hii hapa chini. Labda swali kwenu tunaowatumikia, mna muda wa kutusoma?

Kibiti:


Uchambuzi Wa Kiintelijensia Kuhusu Mauaji Ya [HASHTAG]#MKIRU[/HASHTAG] Kwa Kutumia "Dhana Zinazoshindana" (ACH) ~ Kulikoni Ughaibuni

Jaribio la mauaji dhidi ya Lissu:


Uchambuzi wa Kiintelijensia Kuhusu Jaribio la Kumuua Lissu: Wahusika Kina Nani ? ~ Kulikoni Ughaibuni

Moja ya changamoto kubwa katika kujipachika wajibu kama huo wa masuala hayo mawili ni kwamba wengi wa ninyi wakongwe wa tasnia ya habari ni "wachoyo" wa mirejesho (feedbacks). Shukrani za pekee kwa investigative journalists ninaowafahamu kama Eric Kabendera na Manyerere Jackton ambao humudu kutumia muda wao adimu kutoa mirejesho yao.

Changamoto nyingine kubwa zaidi ni kile ambacho binafsi nakitafsiri kama "anti-intellectualism" inayozidi kishamiri huko nyumbani. Sawa, wananchi wanaweza kuwa sahihi kupoteza imani dhidi ya expertise, hasa baada ya kushuhudia madudu ya wataalam a.k.a "wasomi" wetu katika masuala mbalimbali. However, sio kila mtaalam/msomi ni mbabaishaji. In fact, just because kuna wataalam/wasomi wamefanya madudu doesn't mean usomi/utaalam = madudu. Correlation doesn't necessarily imply causation.

Sasa hiyo "anti-intellectualism" inachangia kwa kiasi flani kuwavunja moyo baadhi ya wataalam/wasomi kutoa mchango wao kwenye masuala mbalimbali, mchango ambao waweza kuwa karibu/sawa/zaidi ya investigative journalism. Kasumba ya "huyu anajifanya anajua kila kitu" or "huyu nae kila kitu yumo" makes it look like "kujua kila kitu" ni kosa la jinai zaidi ya drug dealing. Na ndio maana baadhi ya wataalam/wasomi wajificha as anonymous kwenye kumbi za majadiliano kama JF.

Kwa "traditional media" zetu, investigative journalism ni ngumu kwa sababu wamiliki wengi wa media zetu wanahofia kuikasirisha serikali. Na sababu kubwa za wao kuhofia kuikasirisha serikali ni (a) kuchelea kufungiwa (b) kunyimwa matangazo na serikali, ambayo ndo tegemeo la media zetu za Tz. Kuna lundo la makala za kiuchunguzi zinazozeekea kwenye mafaili au kompyuta kwa vile mhariri anahofia ajira yake.
 
Yes ''Investigative Journalism'' Do they have power to interrogate and summon, Suppose the Authority turn on a deaf ear What can investigate journalism do
Labda nikujibu kwa kiswahili. Jee wale watuhumiwa wa madini wa kilosa(au kilombelo) kulihitajika mandate ya authority? Waandishi hawa hawa waliweza kusababisha ukweli ukajulikana na kuna afisa wa polisi anasubibri kitanzi.
Paskali anaweza kulieleza hili vizuri, ila haki ilitendeka kwa kalamu zao.
 
waandishi nyie njaa tupu mnasubiri bahasha ndio mjaze matumbo yenu
Kama mnavyo subiri zile buk7 muishi. Zamani nilijua ni utani wa JF tuu lakini nilipoambiwa na Naibu waziri mmoja mchepuko wangu kuwa ni kweli kuna malipo nilibaki mdomo wazi.
 
Hapa tunaongelea watu wasio julikana ambao huyu mwandishi Anaweza kuwagundua je anauwezo wa kuwatia nguvuni ama hatiani kumbuka hawa watu wasio julikana wana siraha za kivita hapo ina maana kuna ulinzi mkali na Hatarishi
 
Deo Masakilija kumbe bado yupo sipati picha kazeekaje.. Awe na maisha Marefu ni miaka mingi sijamuona wala kimsikia
 
Leo ni siku ya uhuru vya vyombo vya habari duniani, kama serikali ina nia ya thati ya kuwabaini wasiojulikana, strong media inaweza inaweza kuwasaidia.

Swali ni jee Tanzania, tuna strong media zenye uwezo wa kuisaidia serikali yetu kuwabaini hawa wasiojulikana?.

Kwa upande wa individual journalists, najua Tanzania tuna waandishi wenye uwezo huo, mfano hai ni mimi mwenyenyewe, namfahamu mwandishi mmoja mwenye uwezo huo, nikamuuliza kwa nini asijitolee tuu kwenda polisi kuwasaidia kuwabaini, alinieleza hana tatizo, kujitolea kuwasaidia polisi kuwabaini wasiojulikana hawa, ila ana wasiwasi na polisi wetu kama wana nia ya dhati ya kufanya uchunguzi, maana anahisi, hai polisi, wakilisikia jina la kubwa la wasiojulikana, wataishia kubaki midomo wazi, na kuweza hata kumgeuzia kibao, badala ya yeye kuisaidia polisi, polisi wanaweza kumtia ndani na kumhifadhi jumla ili kumkingia kifua, kubwa la wasiojulikana.

P.
 
Lakini Pasco hao wasiojulikana wameshajulikana Ila wakuwataja hadharani ndio wasiojulikana.
 
Pasco, kwa hiyo waendelee kutamba?
 
Bandiko lileishi miaka2 bado jipya kabisa
 
  1. Ina maana hujui nani kaamuru kuawa Ben Saanane?
  2. Hujui nani kaamuru Tundu Lissu ashambuliwe?
  3. Hujui nani alikuwa nyuma ya utekaji wa Mo Dewji ?
Nakuheshimu kitu kimoja, unatumia verified ID, lakini ukweli unaujua. Tuishie hapa
Kwanza nakushukuru kwa kuniheshimu kutumia verified name. Licha ya kutumia verified name pia mimi ni mwana habari, jukumu kuu la waandishi wa habari ni tell nothing but the truth. Hivyo mimi ni mkweli daima na yote niandikayo humu ni kweli tupu.

Kuamini ni jambo moja na kuwa na hakika ni jambo jingine. Nakuomba mambo ya imani, tuyaache kwenye dini, hapa tuzungumzie vitu vyenye uhakika na sio masuala ya imani.
  1. Ina maana hujui nani kaamuru kuawa Ben Saanane?. Kwanza sina uhakika kama Ben Saanane ameuwawa, wewe ndio unanieleza sasa. Nijuavyo mimi ni Ben Saanane ametoweka katika mazingira ya kutatanisha, mpaka sasa hakuna ajuaye kilichomkuta. Kumbe mwenzetu unajua kuwa kauwawa na una mjua hadi aliyeamuru Ben Saanane kuuwawa!. Una uhakika wa hili?.
  2. Hujui nani kaamuru Tundu Lissu ashambuliwe?. Pia simjui aliyeamuru Tundu Lissu ashambuliwe, kwenye hili la Tundu Lissu, mimi naungana na mamlaka rasmi kuwa Tundu Lissu ameshambuliwa na watu wasiojulikana, na nimeisha andika mabandiko mengi kuhusu shambulio la Tundu Lissu. Vipi wewe mwenzetu unamjua aliyeamrisha Tundu Lissu ashambuliwe, una uhakika?.
  3. Hujui nani alikuwa nyuma ya utekaji wa Mo Dewji ?. Hata aliye nyuma ya shambulio hili mimi simjui, wewe mwenzetu unamjua?. Una uhakika?.
P
 
Majibu yote unayo, sisi watu wazima tunaelewana kwa uandishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…