Je kuna aliyebisha hayo ? Tofauti ni kwamba Imani haiitaji uthibitisho hata bila Imani watu wataamini, tofauti na facts ambazo hata zisipokuwa proven bado ni facts ili kuweza kuthibitisha kwamba ni facts (ni kama sentensi inavyosema kuthibitisha which means they must be proven
Hata Ngw'anamalundi pia ni historical figure katika baadhi ya sehemu ukizingatia historia ya zamani ilikuwa inarithishwa kwa hadithi na nyimbo; na vilevile uwepo wa mtu haimaanishi kila alichofanya ni kweli alifanya kuna exaggarations (mfano tuchukulie Nyerere tu kuna watu walikuwa wanaamini ana nguvu za kichawi na kuna siku alisahau fimbo yake mtu akataka kuichukua ampelekee akashindwa kuibeba), Kuna watu leo wanamchafua kwamba ndio chanzo cha umasikini wetu yote hayo yapo historically kwenye maneno ya watu na kama mmoja wetu angeyaandika yangeweze kuwa ni ukweli...; Kuna watu wanasema Newton aliona Apple inaanguka ndio akawaza kuhusu gravity, kuna wengine wanasema hio ilikuja tu baadae ili kufanya story hii ionekane tamu zaidi...
Na uki base history kwenye Imani yako nadhani ni kufeli hata kabla haujaanza sababu historia haikubaliana kabisa na chanzo ambacho huyu Yesu alikuwa ndio anachotuelezea kwamba ndio chanzo....
Hata kama haiendani kabisa na tunachodhani ndio ukweli haimaanishi kwamba sio kweli wala wewe kuamini haiitaji kuwa proven at all wala kuendena na wengine wanachoamini..., vilevile unasahau kwamba hata historia inaweza ikawa ni distorted hususan kama historia hiyo ipo based kwenye maandiko ya victors...
Hapana ila kwa busara zaidi ni kutafuta na kutumia avenues zote kutafuta ukweli huo.., na ni kosa kubwa sana kuanza na jibu ndio uanze kuthibitisha ukweli badala ya kuanza na blank slate na facts / evidences ndio zikupeleke kwenye ukweli na ukifika sehemu ambapo utagundua umepotea njia utakuwa radhi na furaha kwamba nimegundua hili sio kweli badala ya kutafuta njia ya kuhalilisha uongo sababu tu uendane and what you thought was right....
Nani kasema haina nafasi (even a broken clock is sometimes right) ila nachosema hauhitaji proof ili kuamini / imani ni wewe tu uamuzi wako na ku train akili yako (mind over matter) kuna watu huwa wanatembea kwenye kokoto za moto kwa kulazimisha akili zao kwamba hizo kokoto ni za baridi....
Sasa kwanini utumie darubini (kuangalia vitu vidogo) wakati jambo linaweza kuonekana kwa deeds (matokeo)? Utaona vipi kwamba kumdhuru mwenzako ni sawa ikiwa wewe hautaki akudhuru (ingawa kuna kipindi ilikuwa ni sawa sababu watu wali justify kufanya mabaya kwa kusema kwamba kuna matabaka na watu wote sio sawa) kuna the chosen ones (mfano wana wa Israel) kwahio hao ni sawa kuwaumiza wengine wasio chosen..., Lakini Civilisation has taught us otherwise... (we continously learn and evolve)
Sijapinga Imani (on the contrary) nimesema to each their own.., wewe amini unachoamini ila tusijebadilisha teachings / education ambazo zinatoa wigo wa inquisitive minds ya watu kuhoji bila kuambiwa wanakufuru kwa kuleta indoctrination ambazo majibu yote yapo kwenye kitabu chenye kurasa 1.200 mpaka 1,500