Setfree Apangua Hoja za Atheists

Setfree Apangua Hoja za Atheists

So what is the purpose of living as na atheist you can be serial killer and die peacefully in your bed without worrying anything to be accountable for
The purpose of living ?!!! Hii nilishaizungumzia na nikuulize wewe kwanini unaishi sababu majibu sio sawa kwa kila mtu...

Na kuhusu accountability na kuwa serial killer ? Nilishauliza pia Kati ya Imani / Mungu na Mema kipi kinaanza (in other words are we doing good because its God willing or it is good because its the will of the Gods)?
 
Naamka kila siku na lengo la kutimiza ndoto/ malengo yangu
Naam kwahio kwa hao uliwaita Atheist hawana ndoto wala malengo ? Na mtu hawezi kutenda mema bila kuwa na Hofu ya Mungu (kwamba ataangamizwa)? and if that is the case huyu ni mnafiki sio kwamba anatenda mema sababu ya huruma na its the right thing to do bali anatenda wema ili aje apate malipo mbeleni (and to be mtu huyu ni hypocrite)
 
So what is the purpose of living as na atheist you can be serial killer and die peacefully in your bed without worrying anything to be accountable for
Nilijua tu unaelewa unatafuta tu wasaa utupie na wewe kizungu chako
 
1. Kigezo cha "Kufeki"
Unasema huenda waliweza kufeki harufu au kubadilisha mwili wa Lazaro. Hebu fikiria mazingira ya tukio: Lazaro alikuwa amekaa kaburini kwa siku nne (Yohana 11:39). Kaburi lilikuwa la mwamba, limefungwa kwa jiwe kubwa, na lilifunguliwa mbele ya umati wa watu, wakiwemo wapinzani wa Yesu. Je, inawezekanaje mtu aliyejificha humo kwa siku nne bila chakula, maji, au hewa safi akatoka nje ya kaburi kwa ghafla akiwa fresh?

Halafu, ndugu zake, majirani, na watu wa Bethania walimfahamu Lazaro. Kama ingekuwa maigizo, mbona hakuna hata mmoja aliyesema, ‘Huyu sio Lazaro, huyu ni mtu mwingine’? Watu wa karne ya kwanza walikuwa na akili timamu na walijua maiti ni nini na kwamba mtu mzima hawezi kujificha kaburini siku nne bila kufa.

2. “Stori za Gahawa”
Kama tukio hilo lilikuwa stori za gahawa, kwanini stori hiyo ilienea haraka kiasi cha kwamba hata maadui wa Yesu (Wayahudi wa Kisanhedrin) hawakuweza kuidhibiti? Badala yake, wao wenyewe walikubaliana kwamba muujiza huo ulifanyika na wakapanga njama za kumuua Lazaro ili kufuta ushahidi (Yohana 12:10-11). Kama ingekuwa stori ya kutengenezwa, suluhisho rahisi lingekuwa kuwafichua waongo, si kupanga mauaji ya mtu aliye hai.

3. Kufeki Harufu ya Mfu
Mkuu, unafikiri watu wa kale walikuwa wajinga kiasi cha kushindwa kutambua harufu ya mfu? Maiti, hasa katika joto lililopo Mashariki ya Kati, inaoza kwa haraka sana. Watu wa wakati huo walikuwa na uzoefu wa vifo na mazishi kuliko sisi wa leo. Hawakuhitaji ‘kujifanya’ wananusa harufu mbaya; walijua jinsi maiti inavyooza na inavyonuka.

Zaidi ya hayo, familia yake ilisema wazi: ‘Bwana, ananuka’ (Yohana 11:39). Ikiwa walihisi harufu hiyo, unataka kusema walikuwa wakishiriki katika njama ya kudanganya? Kwa nini dada yake mwenyewe (Martha) alisita kuamini kuwa Lazaro atafufuka kama angekuwa anajua ni maigizo tu?

Mkuu, inawezekana unakataa tukio hili kwa sababu hutaki tu kuamini, lakini kukanusha na kudai ‘labda walifeki’ bila ushahidi wowote ni hoja isiyo na mashiko. Ikiwa watu wa wakati huo walikubaliana kuwa Lazaro alikufa na akafufuka, kwa nini sisi wa leo, walio mbali na tukio lenyewe, tunajiona tuna ufahamu zaidi kuliko mashahidi waliokuwepo?

Shetani anatafuta kutupotosha ili tuangamie pamoja naye katika moto wa milele. Tumpinge kwa Jina la Yesu Kristo. Amen
Mkuu kweli unaweza ukaona plausibility na uwezekano wa kufufuka alafu ukapinga kabisa uwezekano wa such a thing kuwa staged ? Yaani absolutely impossible ?

Ila zaidi ya yote wewe kama unaamini and it looks like you do.., and it makes you happy and gives your life a meaning it would rather be sadistic of me to try and take that away from you (and that is why I normally don't like to engage in such debates) because if the end game will be removing something which is precious from you that will not be a happy ending, even I would not like that.... (One extra miserable person)

Kwahio good on you on your faith.., ingawa kila utakapokuwa unajaribu kupitisha / kubadilisha faith yako kama scientific facts you might encounter me again and again.... thus I ask for forgiveness in advance.
 
Bado wanauliza kwamba kama kila kizuri na kibaya kina mwanzo je nayeye kwenye kuanzisha hizi harakat zote, yeye kaanzishwa nanani.
 
Back
Top Bottom