1. Kigezo cha "Kufeki"
Unasema huenda waliweza kufeki harufu au kubadilisha mwili wa Lazaro. Hebu fikiria mazingira ya tukio: Lazaro alikuwa amekaa kaburini kwa siku nne (Yohana 11:39). Kaburi lilikuwa la mwamba, limefungwa kwa jiwe kubwa, na lilifunguliwa mbele ya umati wa watu, wakiwemo wapinzani wa Yesu. Je, inawezekanaje mtu aliyejificha humo kwa siku nne bila chakula, maji, au hewa safi akatoka nje ya kaburi kwa ghafla akiwa fresh?
Halafu, ndugu zake, majirani, na watu wa Bethania walimfahamu Lazaro. Kama ingekuwa maigizo, mbona hakuna hata mmoja aliyesema, ‘Huyu sio Lazaro, huyu ni mtu mwingine’? Watu wa karne ya kwanza walikuwa na akili timamu na walijua maiti ni nini na kwamba mtu mzima hawezi kujificha kaburini siku nne bila kufa.
2. “Stori za Gahawa”
Kama tukio hilo lilikuwa stori za gahawa, kwanini stori hiyo ilienea haraka kiasi cha kwamba hata maadui wa Yesu (Wayahudi wa Kisanhedrin) hawakuweza kuidhibiti? Badala yake, wao wenyewe walikubaliana kwamba muujiza huo ulifanyika na wakapanga njama za kumuua Lazaro ili kufuta ushahidi (Yohana 12:10-11). Kama ingekuwa stori ya kutengenezwa, suluhisho rahisi lingekuwa kuwafichua waongo, si kupanga mauaji ya mtu aliye hai.
3. Kufeki Harufu ya Mfu
Mkuu, unafikiri watu wa kale walikuwa wajinga kiasi cha kushindwa kutambua harufu ya mfu? Maiti, hasa katika joto lililopo Mashariki ya Kati, inaoza kwa haraka sana. Watu wa wakati huo walikuwa na uzoefu wa vifo na mazishi kuliko sisi wa leo. Hawakuhitaji ‘kujifanya’ wananusa harufu mbaya; walijua jinsi maiti inavyooza na inavyonuka.
Zaidi ya hayo, familia yake ilisema wazi: ‘Bwana, ananuka’ (Yohana 11:39). Ikiwa walihisi harufu hiyo, unataka kusema walikuwa wakishiriki katika njama ya kudanganya? Kwa nini dada yake mwenyewe (Martha) alisita kuamini kuwa Lazaro atafufuka kama angekuwa anajua ni maigizo tu?
Mkuu, inawezekana unakataa tukio hili kwa sababu hutaki tu kuamini, lakini kukanusha na kudai ‘labda walifeki’ bila ushahidi wowote ni hoja isiyo na mashiko. Ikiwa watu wa wakati huo walikubaliana kuwa Lazaro alikufa na akafufuka, kwa nini sisi wa leo, walio mbali na tukio lenyewe, tunajiona tuna ufahamu zaidi kuliko mashahidi waliokuwepo?
Shetani anatafuta kutupotosha ili tuangamie pamoja naye katika moto wa milele. Tumpinge kwa Jina la Yesu Kristo. Amen