dketikai
Member
- Nov 13, 2016
- 26
- 19
Kumetokea mkanganyiko sehemu ya kazi ambapo imebidi nije na uzi huu. Kwa kawaida sehemu hii ya kazi kuna neno gratuity hutumiwa kuwa utalipwa baada ya kufanya kazi kwa miaka miwili yenye mkataba wa mwaka mmoja moja,kwa hiyo ukifikisha miaka miwili unalipwa. Ila mwaka jana kama kawaida tulatumikia mkataba wa mwaka mmoja ambao una gratuity na mwaka ukaisha salama. Hivyo ukabaki mwaka huu mmoja wa 2018 tuumalizie ndio tufikishe miaka miwili tustahili kulipwa. Ila pasipo kutegemea uongozi ukabadili gratuity haikuwepo tena. Likaja neno severance pay nayo ikihitaji miaka miwili. Je mfanyakazi ana haki yoyote na ile gratuity iliyopotezewa? Je nikiamua kuacha kazi kwamba siridhishwi nina haki gani kisheria?