Sevarance pay vs gratuity njia panda

Sevarance pay vs gratuity njia panda

dketikai

Member
Joined
Nov 13, 2016
Posts
26
Reaction score
19
Kumetokea mkanganyiko sehemu ya kazi ambapo imebidi nije na uzi huu. Kwa kawaida sehemu hii ya kazi kuna neno gratuity hutumiwa kuwa utalipwa baada ya kufanya kazi kwa miaka miwili yenye mkataba wa mwaka mmoja moja,kwa hiyo ukifikisha miaka miwili unalipwa. Ila mwaka jana kama kawaida tulatumikia mkataba wa mwaka mmoja ambao una gratuity na mwaka ukaisha salama. Hivyo ukabaki mwaka huu mmoja wa 2018 tuumalizie ndio tufikishe miaka miwili tustahili kulipwa. Ila pasipo kutegemea uongozi ukabadili gratuity haikuwepo tena. Likaja neno severance pay nayo ikihitaji miaka miwili. Je mfanyakazi ana haki yoyote na ile gratuity iliyopotezewa? Je nikiamua kuacha kazi kwamba siridhishwi nina haki gani kisheria?
 
Sina hakika sana ila sidhani km Sheria inalazimisha malipo ya gratuity kwa sasa hasa km unachangia pension funds labda iwe imetajwa kwenye mkataba.

Severance pay hailipwi kwa wafanyakazi ambao mikataba yao imefika mwisho kwa sababu ya muda au aliyeachishwa kwa minajiri ya kinidhamu. Na huwa ni mshahara wa siku 7 kwa kila mwaka uliomfanyia mwajiri kazi mfululizo na kwa kipindi kisichozidi miaka 10
 
Kumetokea mkanganyiko sehemu ya kazi ambapo imebidi nije na uzi huu. Kwa kawaida sehemu hii ya kazi kuna neno gratuity hutumiwa kuwa utalipwa baada ya kufanya kazi kwa miaka miwili yenye mkataba wa mwaka mmoja moja,kwa hiyo ukifikisha miaka miwili unalipwa. Ila mwaka jana kama kawaida tulatumikia mkataba wa mwaka mmoja ambao una gratuity na mwaka ukaisha salama. Hivyo ukabaki mwaka huu mmoja wa 2018 tuumalizie ndio tufikishe miaka miwili tustahili kulipwa. Ila pasipo kutegemea uongozi ukabadili gratuity haikuwepo tena. Likaja neno severance pay nayo ikihitaji miaka miwili. Je mfanyakazi ana haki yoyote na ile gratuity iliyopotezewa? Je nikiamua kuacha kazi kwamba siridhishwi nina haki gani kisheria?
Severance Pay
Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004 inatoa Kiinua Mgongo. Mfanyakazi ana haki ya kiinua mgongo ikiwa amemaliza angalau mwaka wa huduma na mwajiri. Kiinua mgongo Tanzania ni sawa na angalau mshahara wa siku 7 kwa kila mwaka wa ajira uliokamilishwa hadi upeo wa miaka kumi.

Kiinua mgongo hakitalipwa iwapo mfanyakazi ataacha kazi kwa minajili ya utovu wa nidhamu, kushindwa kutekeleza majuku yake kutokana na kuumia na kama atakataa kupangiwa kazi mbadala na mwajiri husika au mwingineyo, au endapo mfanyakazi atakuwa ametimiza umri wa kustaafu au endapo mkataba wa ajira umekwisha au kusitiswa kwa mujibu wa muda wa mkataba. Malipo ya kiinua mgongo hayaathiri haki ya malipo mengineyo ambayo ni stahiki kwa mfanyakazi husika.

Chanzo: § ya 42 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004
 
Hakika uko sawa,na hayo malipo ya siku 7 kwa mwaka uliokamilika ni basic salary ya kila siku bila makato Wala posho
 
Severance Pay
Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004 inatoa Kiinua Mgongo. Mfanyakazi ana haki ya kiinua mgongo ikiwa amemaliza angalau mwaka wa huduma na mwajiri. Kiinua mgongo Tanzania ni sawa na angalau mshahara wa siku 7 kwa kila mwaka wa ajira uliokamilishwa hadi upeo wa miaka kumi.

Kiinua mgongo hakitalipwa iwapo mfanyakazi ataacha kazi kwa minajili ya utovu wa nidhamu, kushindwa kutekeleza majuku yake kutokana na kuumia na kama atakataa kupangiwa kazi mbadala na mwajiri husika au mwingineyo, au endapo mfanyakazi atakuwa ametimiza umri wa kustaafu au endapo mkataba wa ajira umekwisha au kusitiswa kwa mujibu wa muda wa mkataba. Malipo ya kiinua mgongo hayaathiri haki ya malipo mengineyo ambayo ni stahiki kwa mfanyakazi husika.

Chanzo: § ya 42 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004

Shukrani nimeelewa vema
 
Thanks mkuu kwa maelezo yaliyojitosheleza.
 
Back
Top Bottom