Mseza Mkulu,
Hii ngumu kumeza, lakini vumilia tu, ili shetani atutandike inabidi atangaze kuwa hayupo kwa sababu haonekani kwa macho.
Nikirejea kwenye mada yako, nikurudishe nyuma kwenye kitabu cha Hesabu sura ya 22 mpaka 25, nitaeleza kwa kifupi ukipata muda kasome.
Ili ibada ya sanamu(au miungu mingine) itimie mambo manne lazima yatimie
1. Lazima uvutiwe na uzuri wa ile sanamu
2. Lazima ushiriki chakula kilichotolewa kwa hiyo miungu
3. Lazima usujudu kuabudu hiyo miungu
4. Lazima utoe sadaka ya damu kwa hiyo miungu (hapa ni damu za watu, direct or indirect)
Nisikuamishe vumilia, hapo penye kitabu cha hesabu Balaam amepewa dili la kuwalaani wana wa Israel, anapanga madhabahu yake saba ya uchawi inashindikana kuwalaani, maana pale ilikuwa mapambano kati ya madhabahu, madhabahu ya kishetani na madhabahu ya Mungu.
Part 2 jinsi gani sasa ya kupitisha ile laana ambayo imeshindikana kuipitisha kwa njia ya madhabahu, njia ya werevu wa siri pale ikawa ni ngono, anatumwa motto wa kwanza wa kike wa kuhani wa baali na timu yake kwa ajili ya kufanikisha hilo.
Cha kwanza wanaume wanavutiwa na uzuri wa mabinti hawa( hatua ya kwanza ya uabudu sanamu). Wanawavuta kwenye ngono wanaingia laini, wanakaribishwa kwenye sherehe iliyoandaliwa kwa miungu yao tena wanaambiwa kabisa nyinyi kwenye shughuli ya kuabudu hamtakuwepo ila mtashiriki chakula tu (wanaingia laaini, hatua ya pili inakamilika)
Wanazaa watoto nao, wanawaambia inabidi kutoa sadaka ya kuteketeza ya watoto ambayo inahitaji motto mmoja tu wako wanaingia laini( hatua ya tatu na ya nne inatimia) laana iliyoshindikana kupelekwa kwa njia ya madhabahu inakamilishwa na ngono. Ngono ndio njia rahisi ya kukuunganisha na madhabahu zote za kuabudu sanamu.
Ukisoma pale mbele unaona Mungu alivyojawa hasira na mtego huo uliofanikiwa, mpaka kulinganisha hasira yake na alitokuwa nayo Finehasi na kummpa agano la ukuhani wa milele.
Njia rahisi ya kuua imani ya Mungu wa kweli ni ngono tu, maana hapo panakamilishwa uabudu sanamu kwa haraka, kama uamini angalia hatua za Daudi kwa mke wa Uria, zilikamilishwa kama nilivyoainisha hapo juu.
Na kwa wakatoliki wasome kitabu cha Yoshua bin Sira anaeleza wazi kuwa ngono ni kama moto ulivyo kwenye kuni kavu ukishaingia hautazimika mpaka kuni zimeisha, ndivyo ngono ifanyavyo kazi kwenye mwili wako ukiindekeza haitoki mpaka imekuteketeza.
Ngono nje ya ndoa mwisho wake mauaji, kafumaniwa, kajinyonga, katoa mimba, kamtangaza vibaya mbele za watu(katuma picha za uchi wa mwezie), kafilisika, kamnyangánya kigari alichomuhonga, kafukuzwa kazi na moto wake unaanza taratibu ninastress,
Shetani haji bali kuiba, kuvunja, kuharibu na mwisho nikuua, shetani hajawahi kuwa rafiki wa binadamu hata siku moja. Unakumbuka Ayubu mara ya kwanza anamwambia Mungu gusa mali zake atakukufuru, aliposhindwa anasemaje?
Wewe Mungu mali si kitu mambo ni mfupa kwa mfupa, ngozi kwa ngozi hapo lazima akukufuru kwa hiyo anahamia kwenye kumtandika kwa magonjwa.
Kwa wale ambao mnasubiri kuona vitu vya rohoni kwa macho endelea kukusanya laana za kutoka kila upande za kifipa twende, wa wajaluo chukua, za wanyasa beba, za wadigo twende kazi, za kichina kama kawaida, za kimangáti we beba, za kizaramo mia tano mia tano