SGR itasafirisha nini?

SGR itasafirisha nini?

Nadhani ujenzi wa reli ya kisasa ni jambo ghali Sana. Wakoloni walijenga reli kibiashara je SGR inajengwa kibiashara pia? Bidhaa zipi kutoka wapi zitasafirishwa kifaida kwenda wapi?

Sioni mazao ya kilimo, bidhaa za viwandani wala mizigo ya bandari mingi Sana inayohitaji kuyafikia masoko haraka na Kwa wingi.

Ujenzi wa SGR ungeendana na upanuzi wa bandari, mashamba na viwanda. Lakini hata tukipanua bandari, kilimo na viwanda je, masoko ya bidhaa hizo ni akina nani ambao wanaishi wapi?
Itasafirisha MICHEMBE kwenda MISUNGWI
 
Mkuu kwani umesahau jinsi ambavyo tz tukitaka kufanya mradi flani jinsi ambavyo huwa unakuzwa Tena kwa tambo......
2000s songas- tuliambiwa mgao/kukatika kwa umeme ingebaki historia tz....
2010 gasi mtwara- tz mkaa itakuwa hadithi...
2010/16 brt- foleni dar itakwisha kabisa ...
2005 Richmond/dowans/aggreco- tutazalisha mega Hadi kuzidi mahitaji....
Na n.k
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Ukiwafuatisha wanaumiza kichwa sana
 
Nadhani ujenzi wa reli ya kisasa ni jambo ghali Sana. Wakoloni walijenga reli kibiashara je SGR inajengwa kibiashara pia? Bidhaa zipi kutoka wapi zitasafirishwa kifaida kwenda wapi?

Sioni mazao ya kilimo, bidhaa za viwandani wala mizigo ya bandari mingi Sana inayohitaji kuyafikia masoko haraka na Kwa wingi.

Ujenzi wa SGR ungeendana na upanuzi wa bandari, mashamba na viwanda. Lakini hata tukipanua bandari, kilimo na viwanda je, masoko ya bidhaa hizo ni akina nani ambao wanaishi wapi?
Hayo malori yote yanayotuharibia barabara yanabeba nini
 
Kwani unaharka ya nini, subiri ijengwe na kumalizwa ndio utaona mazao watu yakisafirishwa!
 
Hayo malori yote yanayotuharibia barabara yanabeba nini
Malori makubwa yapo duniani kote hata ulaya na marekani yapo lakini barabara zao haziharibiki kwakuwa barabara zao zinafahamika uimara wake na uzito wa mizigo inayotakiwa kupitishwa. Tanzania tuna mizigo michache sana yenye uzito mkubwa unaohitaji reli. Mara nyingi hatujengi reli ili kuzuia uharibufu wa barabara bali tunahitaji reli ili kubeba mizingo mingi kwa wakati mmoja. Hiyo mizigo mingi na mizito sana isiyofaa kusafirishwa kwa barabara tunayo? itatulipa gharama za kujenga reli? Au tutalazisha mizigo yote ipite kwenye reli kwa kupiga marufuku malori? Je, ajira za malori zitakwenda wapi?
 
Back
Top Bottom