Ninarudia, wewe ni mpumbavu sana na pupa kabisa wewe. Serikali jukumu lake kikatiba ni kukusanya kodi za wananchi na kuwekeza katika huduma za wananchi ikiwemo miundombinu ya barabara, reli, meli na Angani. Kutengeneza faida sio lengo na kipaumbele cha serikali yoyote ile. Jukumu la serikali ni kuweka mazingira wezeshi ya kibiashara ili watu binafsi wafanye biashara, mazingira hayo wezeshi ni:
1)Barabara zinazopitika kipindi chote
2)Reli yenye kusafirishwa mizigo mizito kwa gharama nafuu
3) UMEME wa uhakika kwa gharama nafuu
4) Mtandao mzuri wa usafiri wa Anga, ndani na nje ya nchi
5) Sera na mazingira rafiki kwa biashara
6)Amani na usalama.
Sasa wewe umebaki kupiga domo hata hujui ubalozungumza. SGR itashusha sana gharama za usafirishaji kutokana na kwamba
1) Tunajenga kwa pesa yetu, hivyo hatutolazimika kurudisha mkopo pamoja na riba.
2) Reli ya umeme gharama za uendeshaji ziko chini sana ukilinganisha na diesel, serikali itaweza kutoza nauli ndogo kwa mizigo na abiria, hivyo kuongeza chachu ya kufanya biashara.
3) Serikali haitoagiza diesel kwa ajili ya hizi train, hivyo kusave pesa ya kigeni.