Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kuna siku nilikuwa natakiwa kusafiri kuelekea Dar es Salaam kutokea Morogoro. Wakati nakata tiketi ya SGR mtandaoni nikiwa Morogoro, badala ya kuandika Morogoro kama kituo cha kuondokea, nikaandika Dar es Salaam. Hivyo, tiketi ikawa inasomeka kutoka Dar kwenda Morogoro ingawa nilitakiwa kusafiri kutokea Morogoro kwenda Dar.
Baada ya kufika kwenye kituo cha SGR Morogoro wakati wa ku-scan tiketi yangu ili kui-print, ndipo wakaniambia mbona inaonyesha Dar es Salaam kwenda Morogoro? Na wewe unataka kwenda Dar es Salaam. Nikawaambia naomba nibadilishieni route isome Morogoro to Dar es Salaam kama nilivyokusudia, wakasema hapana haiwezekani.
Kwasababu nilikuwa na haraka, kuna kazi nilitakiwa kuifanya Dar kisha nirudi Moro ikabidi nikate tiketi nyingine. Nimefika Dar nimefanya Mitikasi yangu haraka ili niwahi tena kituoni kwenda kurekebisha tiketi yangu ambayo nilikata asubuhi Morogoro ambayo ilionyesha route ya Dar – Moro kwa lengo niitumie wakati wakurudi nikaambiwa tena haiwezekani eti kwasababu imetoka kwenye mfumo.
Sasa kama ili ionekane tiketi imetumia lazima iwe scaned na yangu haikutumia kwanini sikurejeshewa pesa? Kama sio urasmu ni nini hasa?.