SGR na uwekezaji mkubwa wa viwanda Tabora, Dodoma, Singida, Morogoro, Shinyanga

Nakubaliana na kauli hii, lakini pamoja na kuwa swala kuwa letu, serikali haiwezi kamwe kujiondoa katika hatua hiyo ili kufanikisha hizo shughuli za wananchi, kwa mfano ruzuku ya mbolea na maswala mengi mengine katika shughuli hizo.
Sasa labda ungeainisha baada ya Sirikali kuwekeza hivyo vikubwa ambavyo Mimi na wewe hatuwezi, hayo mengine ambayo yamekuwa kikwazo kwako kufungua kiwanda au kulima ni nini.useme Una Ardhi sehemu fulani, na umeshindwa kulima sababu ya mbolea au hayo mengine.
 
Ndugu yangu inashangaza sana mpaka Karne hii Wenye mitaji bado wanachuana na wajasiliamali wadogo wadogo kununua bidhaa na kuleta kuziuza huku, Badala ya kuimport mashine za kuzalisha bidhaa hizo ili tuzalishie nyumbani wawo wabaki wazalishaji wakubwa ikiwezekana exporter wakubwa, Bado tunaagiza toothpick na mianzi tunayo,embu fikiria muanzi mmoja unazalisha toothpick ngap?, Bado tunaagiza maelf na maelf ya pampas na mali ghafi zipo na inasemekana hivi vitu huzalishwa na Medium mashine kabisa unafikiri huyo Mkulima utamkomboa vipi?
 
Tatizo kubwa ninaloliona nikuanzishwa huku tukiwa na malengo yale yale waliyokuwa nayo wakoloni kusafirisha Rasilimali na kuingiza bidhaa kutoka kwa wenzetu, Tujikite na kujiimalishe angalau katika kuongeza thamani Rasilimali zetu ili kuongeza base ya faida za uwepo wa reli hii hapo ndipo itagusa sector nyingi na uchumi wa watanzania wengi.
Pili nakubaliana na wewe tatizo kubwa la nchi yetu ni Management, Plan tunakuwa nazo nzuli na tatizo linakuja kwenye uendeshaji kwenye hili nazilaumu Mamlaka zetu za kuwajibishana tunaleta uswahili wa kuoneana aibu huku watu wengi watanzania wengi wakiumia.
Tatu wananchi wenyewe hakuna mfatiliaji kwanza ufisadi, Wizi, na uhuni uhuni tunauita ni ujanja, mtu mwizi utasikia mswahili anasema jamaa mjanja mjanja sana hii inawafanya hawa watu waone sifa kutuibia, Mwizi aitwe mwizi, Fisadi aitwe Fisadi unajua hata kumita mtu kwa sifa zake mbaya ni hukumu tosha na inaweza changia kumbadilisha mtu na jamii
 
Matumizi yapo hasa mizigo inayopita ndani ya nchi kwenda nchi jirani hususani DRC ambayo inabeba asilimia takribani 41 ya mizigo inayopita ktk bandari zetu.

Katika hili umuhimu wa kupereka SGR bandari ya Kigoma/Kigoma una pana kiuchumi kuliko Burundi ama Rwanda
 

Ni aibu

Vyuo vyetu

Elimu yetu ifinyangwe kuwajenga vijana kuona na kutafsiri fulsa lukuki ktk uzalishaji kupitia viwanda vidogo na vya kati..

Lakini mazingira wezeshi ktk mifumo ya compliance za kisheria-Kodi,Leseni,Vibali etc
 
Nakubaliana na kauli hii, lakini pamoja na kuwa swala kuwa letu, serikali haiwezi kamwe kujiondoa katika hatua hiyo ili kufanikisha hizo shughuli za wananchi, kwa mfano ruzuku ya mbolea na maswala mengi mengine katika shughuli hizo.
Hatuwezi kujikomboa kwa kutegemea kuagiza mbolea toka nje kama ilivyo kwa Sukari..

Tujenge uwezo zaidi kwa wazalishaji wa ndani..Tuwape nafuu na incentives kitita..

Viwanda kama MINJINGU FERTILIZERS vilindwe kwa wivu mkubwa..

Kama ambavyo tunapswa kufuta uhuni unaozuia kuuzwa kwa viuatirifu vinavyozalishwa na kiwanda cha Kibaha chini ya NDC (Kilichojengwa na Wacuba)..Malaria inapaswa kuwa historia ktk nchi
 
Hilo la mizigo ni lako, sisi tuko kwenye abiria ambao wanaotushangilia na ndio wapiga kura wetu.
 
Nianishe nini wakati inaonyesha tayari umeelewa ninacho zungumzia mkuu 'August'?

Serikali ina wajibu, tena mkubwa sana kwa wananchi wake katika maswala ya shughuli zao. Hata kama si kama hiyo ruzuku ya mbolea iliyo elezwa hapa, kuna mambo mengi sana ambayo serikali ni lazima iwemo; hata kwenye masoko ya bidhaa, sera za kuunga mkono shughuli hizo za wananchi, n.k..
 
Mkuu 'FUTURE PLAN', sijui kama hili uliloweka hapa ni kweli; kwamba reli inajengwa kwa malengo yale yale ya wakoloni. Inawezekana hii ikawa ni hisia zako tu zinazochangiwa na hao hao viongozi kutokuwa na uwezo wa kuyasemea mambo kama haya ili wananchi wajue misingi ya miradi mkakati kama hii ya usafirishaji.
Hata hivyo kumekuwepo na jitihada za muda mrefu tokea tupate uhuru kuyabadili hayo malengo ya kikoloni, hata kama juhudi hizo zimekwama kwa sababu mbalimbali.
Uhitaji wa reli hii siyo swala tena la kuifikiria kuwa na malengo hayo hayo waliyokuwa nayo wakoloni.
Tatu wananchi wenyewe hakuna mfatiliaji
Hili la wananchi wengi kulazwa usingizi na CCM na kuwageuza kuwa washangiliaji wa maovu wanayofanyiwa wenyewe ni jambo la kusikitisha sana kwa nchi yetu.
 
Sijasema popote pale katika andiko langu kwamba tuwe 'tegemezi' kwa kitu chochote kilicho ndani ya uwezo wetu kukifanya, kama hizo mbolea , sukari na mengi mengine.
Lakini pia ungeweza pia kukumbuka kwamba juhudi zetu za kuzalisha mbolea, sukari na vinginevyo hatujawahi kuzifanya na kwamba hatuwezi kutoendelea kuzifanya. Hili siyo jambo geni hapa kwetu,; tofauti tu inayo jitokeza ni wakati tunapokuwepo na serikali kama hii inayotegemea kuwa maendeleo ya nchi yetu yataletwa hapa toka nje. Hawa ndio wanao tudidimiza zaidi na kuua kabisa moyo wa uthubutu wetu kujifanyia mambo yetu ili nchi yetu ipate maendeleo ya kweli.
 
Hakuna haja ya kupima upya namna ya kuwekeza viwanda; wao wafuate plani alizoasisi Nyerere tu mradi waziboreshe kuendana na wakati tu. Kama hawazijui au hawazikumbuki, mimi nitawajulisha.

Hawa watu wanapenda tuwaone ndio vipanga wetu. Kumbe buana😎😎😎😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…