KERO SGR rekebisheni muda wa Safari, mnapoteza abiria

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hivi tren ikikuacha unaikimbiza na nini ili upande maana basi tunalikimbiza na toyo na linasimama napanda zangu polepole ?
 
Mie nikajua labda tren ya kuondoka saa 12 imeondoka saa 1.
Kwa Hapo usiwalaumu SGR, kata tiketi yako online mapema, unakuwa na uhakika wa safari, mie nilikata tiketi tren ya kutoka moro kuja dar ya saa 2 na dk 50asubuh, kwa kuwa tiketi nilikata toka jana yake kwenye mtandao, siku ya safari nilifika stesheni saa 2 na nusu hivi, saa 2 na dk 50 safari ikaanza.
 
Unahisi wao hawalijui hilo ? Hi nchi we acha tu vitu vya umma vinahujumiwa sana

Kuanzia sa 2 asubuhi Hadi sa 8 mchana ndio muda ambao Kuna abiria wengi wa Dar to Moto na ndio muda ambao treni hakuna lazima watu wapande mabasi
 
tofauti ya nusu saa na masaa mawili

Sijakuelewa, mimi nimezoea kuondoka nyumbani saa 9 ili nipande basi saa 9:30, sasa huo uvivu ni upi! Mimi ninamuona anayelalamika kuwa saa 12 ni mapema sana kuwa ni mvivu.
 
Unahisi wao hawalijui hilo ? Hi nchi we acha tu vitu vya umma vinahujumiwa sana

Kuanzia sa 2 asubuhi Hadi sa 8 mchana ndio muda ambao Kuna abiria wengi wa Dar to Moto na ndio muda ambao treni hakuna lazima watu wapande mabasi
Wenzako tunapanda treni Dar / Moro saa 12 nafika Moro mapema napanda basi saa nne niko Dodoma.
 
Mbona Ndege huwa hatuuliza maswali haya?
Ndege watu hawaulizi kwa sababu wangeweka saa kumi na mbili asubuhi na saa tatu, na nyingine saa tisa na saa kumi na mbili
 
Online unakata vipi mkuu ?
 
Sijakuelewa, mimi nimezoea kuondoka nyumbani saa 9 ili nipande basi saa 9:30, sasa halo uvivu ni upi! Mimi ninamuona anayelalamika kuwa saa 12 ni mapema sana kuwa ni mvivu.
Kuamka saa 9 inahitaji effort kubwa, pamoja na kujinyima usingizi wa optimum masaa 7 ili akili ifanye kazi sawasawa. Life is about minimizing the effort required in doing things. Usemi kuwa nimezoea shida hauna uhalisi, bali watu wanavumilia shida. Kwa hiyo TRC hawapaswi kuweka ratiba ambazo zinahitaji watu waweke effort kubwa ya kuamka pasipo sababu za msingi. TRC wana sababu zipi za msingi za kuondoka saa 12 asubuhi wakijua watu itabidi watumie effort kubwa kuamka saa 10 alfajiri ili waende stesheni na waiwahi train?

Katika kupanga mambo hata kutengeneza kiti chako tu cha kukalia, kuna element inaitwa egonomics. Sijui kama hawa kina Kodogosa wanajua hivi vitu.

Kama nimekuacha mbali acha tu usiko comment. Hii inaweza ikawa sio level yako ya shule.
 
Wewe sio msafiri serious.
.tunaishi dar tunafanya kazi Moro.
 
Si mpande Ngorika??? Hata saa hizi Unplikuta Shekilango sijui Mbezi...
Maudhi mengine tunajitakia wenyewe
 
Hivi tren ikikuacha unaikimbiza na nini ili upande maana basi tunalikimbiza na toyo na linasimama napanda zangu polepole ?
Ukimbize treni ya SGR ikiwa umechwa? Labda uwe Mpare. Maana utaingia gharama mara tano ya bei ya ticket na utafanikiwa kuipata, ikiwa imeshafika Morogoro!
 
Sijakuelewa, mimi nimezoea kuondoka nyumbani saa 9 ili nipande basi saa 9:30, sasa huo uvivu ni upi! Mimi ninamuona anayelalamika kuwa saa 12 ni mapema sana kuwa ni mvivu.
amesema anatakiwa aende kukata ticket saa 10 kama hana ticket halafu safari saa 12
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…