Wajasiriamali wa tz hawataendelea mpaka wabadilishe mindsets. La sivyo umaskini utaendelea tu. Kila kijana siku hizi nikimuuliza ni kwa nini unakaa tu kijiweni huna biashara anakwambia kama ningepata milioni 50 ningeanzisha biashara safi kabisa. Baada ya miezi kadhaa niende pale toyota tanzania nivute toyota land cruiser! Tunaishi katika material world kila mtu anataka vitu vya kifahari wakati hawana hela. Matajiri karibu wote duniani walianza from scratch na kupanda juu, Bill Gates, Mark Zakabegi, Reginald Mengi, Joseph Mfugale wa peacock, n.k. Swala jingine vijana wanakwambia eti nikianza na mtaji mdogo itachukua muda kuwa tajiri, sasa wewe tokea ukiwa na miaka 20 unasubiria hiyo milioni 50 na leo una miaka 30 bado hujaipata umekaa kijiweni unaisubiria, miaka yote hiyo kumi kama ungeanza kidogo si ungekuwa tajiri tayari sasa! Tatizo jingine vijana wanasema kama akianza na biashara ya kuuza juice anaogopa watu watamcheka, sasa wewe ukiogopa kuanzisha hiyo biashara ya juisi na kukaa kijiweni, hao watakaokucheka kwani wanakupaga hela ya kujikimu kimaisha mpaka uogope kuchekwa nao?? Watanzania tuache visingizio la sivyo tutaendelea kuwa maskini.
Hakuna mzungu, mchina, mhindi wala mtu yeyote atakayekuja na kukuboreshea maisha yako zaidi ya wewe mwenyewe. Kusubiria serikali ikufanyie mambo, utasubiri milele na milele. Wengine wanasema vijana hawawi matajiri kwa sababu ya ufisadi! Mimi sitetei ufisadi but ktk kila nchi duniani ufisadi upo hata china ambako wanaua watuhumiwa wa ufisadi, bado ufisadi unaendelea tu. Mimi naishi finland ambako ni nchi kila mwananchi ana maisha poa sana but bado kuna ufisadi pia. Ishu si ufisadi ila ni wewe mwenyewe kutumia fursa ulizonazo zikunufaishe. Tuache visingizio jamani. We uko radhi utumie laki moja kula nyama choma na bia badala ya kuanzisha kibanda kidogo cha juisi. Kama unaogopa kuuza wewe mwenyewe, weka kijana akuuzie hizo juisi basi.