Shaa, Langa na Witness walipendelewa Coca Cola Pop Star ila mimi Masqo(Deo Kisandu) nikaachwa

Shaa, Langa na Witness walipendelewa Coca Cola Pop Star ila mimi Masqo(Deo Kisandu) nikaachwa

hospital.gif
kwa kwa kwaaaa we jamaa una dhambi saana wallah!!!!
 
Mwezi unaandamwa tena leo. Atakayekuwa karibu yake aje na mrejesho kesho kwa yatakayomsibu.
 
Wabongo bhana,mwenzenu anashusha facts zinazomuhusu alafu mnamtupia madongo
 
Huyu Ni Mtemi Wa Watemi
Mwalimu Deo Kisandu the greatest Mwalimu of all time
Umejaribu kumuelezea lakin kuna sifa moja umeacha,
Huyu ndio yule ambae akimiss kugegeda (hapa nimetumia tafsida, ila ye hatumiagi) basi hutangaza hadharani na kudai kua ni haki yake
 
View attachment 652459
SEVEN na SALAMA JABIR WALINIBANIA USHINDI WANGU WA COCA COLA POP STAR MWAKA 2004 NA KUWAPA SHAA,LANGA na WITNESS LAKINI DUDUBAYA ALINIACHA HOI.

Mashindano ya East Africa Coca Cola Pop Star yaliyofanyika Dar es Salaam mwaka 2004 Mwenge, Mimi Deogratius Kisandu kwa jina la kisanii "Masqo" nilikuwa mshiriki wa mashindano hayo na wakati huo tayari nilikuwa na Tract yangu "Nimepata demu" ikiendelea kupata promo.

Majaji walikuwa ni watangazaji wa East Africa Radio Madam SEVEN na SALAMA JABIR. Washiriki tulikuwa wengi sana wakiwemo wale Soul 'N' Faith, mimi ilipofika zamu yangu niliwahi ukumbini na kundi langu nikaimba wimbo wangu nilioandaa, kama kawaida ya Salama akacheka tu kwa chini SEVEN akamwambia huyu si ndo Masqo mwenye wimbo Nimepata Demu? wakanong'onezana kisha wakanambia unaweza kwenda ila kafanye mazoezi tena.
Ilikuwa ukisha maliza kuimba hurudii tena, mimi nikajifikira yaani nimeimba vizuri halafu nikafanye mazoezi tena,

nikaona hapana nikaenda kuchukua Coupon upya nikapanga foleni tena. Nikasikia wambeya wanamwambia Salama na Seven kuwa Deo Kisandu anarudia tena lakini hakujali, basi ikafika zamu yangu tena, waliponiona walicheka halafu Seven akamwambia salama huyu si amejirudia tena, Salama akasema hebu tumuache ajaribu tena ila hatumuchukui maana tayari ana wimbo una unapigwa radioni. Basi nikaimba tena wakanambia umeimba vizuri kasubiri majibu.

Baada ya Usahili wa wote tulikaa nje huku tunapata Burudani ya Mziki kutoka kwa Bwana Misosi na baada ya kutangaziwa sikusikia jina langu kabisa tukasikia tu Sarah (kwasasa Shaa), Langa na Witness na wengine nimewasahau ambao walienda Top 5 kama sijakosea.
Mziki ni uvumilivu na subira na kujipanga upya mara kwa mara lakini tamasha hili nilitakiwa kushinda kabisa maana niliimba Vizuri mno, lakini Seven na salama walibana.

DUDUBAYA.

Siku hiyo hiyo tullitoka na mshikaji wangu mmoja tukaenda Bongo Record kwa PFunk ili tukapate Lebel lakini tulipofika kwa PFunk ofisini hatukupata nafasi ya kumuona PFunk, tuliondoka zetu mpaka kwa Dudubaya tukamkuta kwake (Sinza) akatukaribisha tukakaa na kupiga stori na kumweleza adhima yetu, lakini hata yeye alikuwa juu ya mawe tu kama sisi hivyo hakuonesha hata nia ya kutusaidia kimtindo mpaka tunaondoka.

DEOGRATIUS NALIMI KISANDU.
16 Desemba 2017.
Ticha hauna hata ka picha hivi ukiwa stejini siku hiyo tukuone?
By the way tuwekee basi huo wimbo wa Nimepata Demu tuupakue, inaweza kukutangaza zaid
 
Umejaribu kumuelezea lakin kuna sifa moja umeacha,
Huyu ndio yule ambae akimiss kugegeda (hapa nimetumia tagsida, ila ye hatumiagi) basi hutangaza hadharani na kudai kua ni haki yake
HAHAHA KUNA SIKU NILIMGOOGLE MCHIZI NIKIWA NATIZAMA PICHA NDIYO NIKAKUTANA NA HIZO SCREENSHOT TOKA FB JAMAA ANASEMA NI HAKI YAKE.
DAH NILICHEKA KINOMA
 
mbona deo kisandu anasakamwa sana humu? Kama kuna mtu ana ugomvi nae si aseme? Utafikiri kawachukulia madem zenu duh. Kwa kweli sijui chanzo cha huyu deo kusutwa namna hii tatizo lake nini tuelewesheni tujue
 
Huyu jamaa kapotelea wapi?

#MaendeleoHayanaChama
Ameshapanda pipa kitambo kwenda Marekani kwa baba yake Nalimi Curtis, ambaye ni Mmarekani Mweusi.

Sema kwa sasa hana nafasi ya kuingia humu jukwaani kutokana na kutumia muda wake mwingi kumfukuzia Malia Obama, ambaye ni mtoto wa Rais Mstaafu wa nchi hiyo.
 
Back
Top Bottom