Shabibiy: Nilinunua basi langu la kwanza nikiwa na miaka 19. Asema mafanikio yake siyo ya kurithi

Shabibiy: Nilinunua basi langu la kwanza nikiwa na miaka 19. Asema mafanikio yake siyo ya kurithi

Hivi kunatajiri asie mjua mganga wa kienyeji?kwa kukaa Kaa zangu tz na viunga vyake

Hakuna watu wa ndumba,watoa kafara,majambazi,wauza madawa ya kulevya,ndovu,kama matijiri

Watu wenye ela hua wanasiri sana za umafia,uzurumati,ndumba nk

Hua nacheka sana na zile story za backresa alianza kutembeza mikate,mengi alikua muuzaj magazeti kwenye magari
 
Mfanyabiashara anayemiliki Mabasi ya Shabiby, Ahmedy Shabiby ambaye pia ni Mbunge wa Gairo amesema alifanikiwa kununua Basi lake la kwanza akiwa na umri wa miaka 19 kutokana na kufanya kazi kwa bidii na kusisitiza kuwa hakuna mbadala mwingine wa mafanikio zaidi ya kufanya kazi kwa bidii.

Shabiby amesema wakati anasoma alikuwa akijishughulisha na biashara ndogondogo na kilimo jambo lililomfanya akiwa na umri wa miaka 19 aweze kununua basi lake la kwanza la kusafirisha abiria.

Shabiby ameongeza kuwa Watu wengi wamekuwa wakidhani mafanikio aliyoyapata yametokana na kuzaliwa kwenye familia ya kitajiri na kurithi mali jambo ambalo amesema sio la kweli bali siri ni kufanya kazi kwa kujituma na kwa bidii bila kukata tamaa.
Atutajie hizo biashara ndogo ndogo
 
Back
Top Bottom