Mimi ni mkazi wa gairo nimefanyakazi kwa shabiby kwenye miaka 90 mwishoni.jamaa ni mpambanaji hakuna uchawi wala pembe za ndovu.
Shabiby aliacha shule kidato cha 2 akaingia shambani kulima mahindi huku akianzisha biashara ya kuuza mafuta kwenye videbe,mtaji ukakua akaanzisha kijisheli pale gairo na wateja wake wengi wakiwa ni wakulima wa mahindi wenye matrekta.
Nikweli baada ya muda mfupi akanunua basi bovubovu akalikatabari na akaanza safari za mpwapwa,basi mpwapwa alipiga hela sana na akaanza kununua chases mtumba za scania na volvo.pale kwake gairo kwenye shell akafungua gereji kwa ajili ya kutengeneza body za mabasi kipindi hicho mabasi ya yutong bado hayajaingia.na wafanyakazi wa kuunda bodi aliwatoa kenya akawaleta gairo hiyo ilikuwa kwenye 2004-2005 hivi,kwahiyo akawa na mabasi zaidi ya 10. Na alilishika soko la abiria karibia wote wa dodoma= dar,dodoma- mbeya na dodoma -arusha kupitia chalinze.
2000 mwanzoni akafungua shell nyingine dodoma mjini pale round about ya makole na wakati huohuo ana trekta kama zaidi ya 15 analima mahindi kibaigwa na .kwahiyo kwa kifupi utajiri wa shabiby hauna makandokando kwasababu anaanza 0 namuona kwahiyo sishangai huku 100 alikofika.
Utajiri uliomfanya awe juu zaidi ni mafuta,kipindi hicho alikuwa anauza mafuta kwa bei ya chini sana kiasi kwamba wateja walikuwa wanapigana vikumbo kwenye shell zake.Haina maana kwamba alikuwa anachanya na mafuta ya taa NO! Sijui alitumia mbinu gani kupata mafuta kwa bei raisi,kumbuka kipindi hicho hakuna EWURA.
Bado akajenga hotel MORENA iliyopo dodoma.
Haya ndio niliyoyashuhudia wakati nafanyakazi kwake kama kuna mengine nyuma ya pazia siyajui.
Sent from my SM-A105FN using
JamiiForums mobile app