Wewe unaweza kuchukulia tukio hili kama ni la kawaida, unacho sahau wazungu wasio penda penda Waafrika na Continent lenywe wanaweza kuanza kujenga hoja kwamba Tanzania si nchi salama kwa wachezaji wa mpira kutoka Ulaya, tukajikuta tunapigwa vita
/propaganda za kutuharibia sifa kimataifa kutokana na ujinga wetu wa kushabakia uwenda wazimu wa mtu mmoja. Nyie mnafikiri kwa nini gazeti moja la Uingereza lilitangaza kwamba Dar ni kijiji cha wavuvi mnafikiri propaganda hizo ni za bahati mbaya - je, wakipata tetezi kwa kile kilicho mtokea Rooney uwanjani mnafikiri tabloid za Uingereza zitakuja na stori gani, si ndiyo itakuwa balaa.
Inakuwaje mtu anaruka uzio anamkimbilia Rooney na Walinzi wanamwangalia tu, wanakuja kuzinduka amekwisha mvaa Rooney, je, kama angekuwa amerukwa akili akamfanya lolote Rooney Wizara ya michezo ingetoa ufafanuzi/maelezo gani - haya si mambo ya kuchukuliwa lightly hata kidogo. Angalieni tena picha za tukio, je, nyuso za wachezaji/wageni zinaonekanaje? kuna anaye tabasamu au kucheka, hakuna; angalia mkono wa kulia wa Rooney unaonekanaje - alikuwa kwenye harakati za kujihami, actually anamsukuma jamaa na uso ameukunja kabisa!! Wamekasirishwa na tukio hilo hata kama awasemi dhahili kwa hivi sasa lakini body languages zao speaks VOLUME.