Shabiki huyu kanichosha khaaa....

Shabiki huyu kanichosha khaaa....

Aisee ungemmwagia mbegu huyo jamaa ili akuheshimu.
 
Ungemwambia Brazil lilikuwa koloni la Ureno baada ya hapo kama hatokuelewa basi muulize elimu yake
 
Mjinga uyo
Niliutambua uwezo wake kimaarifa ndio maana nilijifanya kutokujua kitu ili aendelee kunipa udambwi dambwi.
Baadae akaniambia wale wachezaji wa Uholanzi wanatokea Itali eti kwa kuwa jezi walizokuwa wamevaa zilikuwa na nembo ya Itali. Nikamwitikia ahaa.
 
Nilikuwa naangalia game kati ya Ureno na Uholanzi ambayo imeisha kwa Ureno kufungwa tatu bila.

Sasa baadae akaja jamaa mmoja akakaa karibu nami (wakati huo Ureno washakufa 3 na mimi ndio timu yangu) akaniuliza Itali wanacheza? Nikamjibu hapana ni Uholanzi na Ureno,akasema ahaa.

Mara Ronaldo akapumzishwa na nafasi yake kuchukuliwa na Moutinho,sasa huyu shabiki akawa ametamka Coutinho kisha akasema Ureno Brazil zimepakana(hapa nikajisemea moyoni labda kaona majina yanataka kufanana japo yeye aliona yamefanana ndio maana kasema hizi nchi zimepakana)kuhusu location akanifanya nikachoka mwenzenu.

Aliponichosha zaidi ni pale aliponiambia kuwa hizi nchi zote zinatoka bara la Asia,hapa sasa ndio nilitamani hata kuondoka khaaaa.(Lakini nikajiuliza ama pengine continental drifting imefanyika tena ila mimi ndio sijui?

Wakati mimi najua Brazil iko bara la A.Kusini na Ureno ipo Ulaya.
[HASHTAG]#APAMBANENAHALIYAKEETU[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom