Full charge
JF-Expert Member
- Mar 1, 2018
- 1,678
- 1,617
#TANZIA: Shabiki wa Klabu ya Simba, Mjata Mjata, amefariki Dunia wakati akipatiwa matibabu mkoani Tanga. Mjata alikuwa mmoja wa wadau wa soka waliokuwa na mchango mkubwa katika kukuza mchezo wa soka, na hasa kupitia upendo wake kwa timu ya Simba SC.
Mjata Mjata ni miongoni mwa mashabiki waliojipatia umaarufu kupitia kipindi cha mashabiki #KipengaXtra cha East Africa Radio na EATV na alipewa jina la utani la #Mpakamafuta, pia alikuwa mwanachama wa EATV Jogging Club.
Kwa taarifa za awali Mazishi ya Mjata yatafanyika Kesho Februari 25, 2025 nyumbani kwao Korogwe Tanga.
Familia ya wafanya biashara wa Mwenge Dar es salaa enao ambalo Mjata Mjata alikuwa anafanyia shughuli zake za kila siku wameandaa utaratibu wa kuchangisha michango ili kufanikisha safari ya kwenda Tanga kwenye mazishi pamoja na kutoa pole kwa familia.
Kwa michango na utaratibu wa kusafiri tuwasiliane na Rajabu Athumani Namba yake ya simu 0678-252728.
Pumzika kwa Amani Mjata Mjata.