TANZIA Shabiki Maarufu Wa Simba SC Mjata Mjata maarufu kama mpaka Mafuta Afariki Dunia

TANZIA Shabiki Maarufu Wa Simba SC Mjata Mjata maarufu kama mpaka Mafuta Afariki Dunia

Rip kamanda dah aisee nilikuwa nampenda sana hoja zake brda
 
Nmesikitishwa sana na kifo chake.. Mjata Mjata kuna muda alikua hapaki nafuta anaongea fact moja kati ya mashabiki wa Simba ambao hawakua na mihemko... Ila gafla sana aisee! Apumzike kwa amani
 
Nilisikia kuwa Anaumwa.
Nilikuwa nakaa Mikocheni mala nyingi nilikuwa napita mwenge na akina Kampista, Gosa nk.

Jamaaalikuwa mtu poa mno.
Alijua kuipenda simba na kuoenda mpira.

Pia alikuwa mkweli, kwenye kusifia anasifia na kwenye kuponda anaponda.

RIP. M J A TA M J AT A.
 
RIP Mjata.
Ile sauti yake ntaikumbuka sanaa. [emoji24][emoji24][emoji24]
 
Inasikitisha Sana ,Mjata mjata alikuwa mchambuzi mzuri sana kwenye kipenga extra ,mpambano unakuwa mkali studio akiwa na nabii meja na mzee Mwenda.
 
Hivi yule jamaa wa yanga analiekuwa analia anasema "sisi mashabiki ndio tunaoumia, kwani hujaona pale..." yupo wapi na anaitwa nani?
Yule ni Steve "Kulialia",alishahamia Azam ambako walimpa ajira kabisa,sas hivi anatembea na makamera viwanjani
 

Attachments

  • Screenshot_20250224-181946.png
    Screenshot_20250224-181946.png
    1.1 MB · Views: 1
#TANZIA: Shabiki wa Klabu ya Simba, Mjata Mjata, amefariki Dunia wakati akipatiwa matibabu mkoani Tanga. Mjata alikuwa mmoja wa wadau wa soka waliokuwa na mchango mkubwa katika kukuza mchezo wa soka, na hasa kupitia upendo wake kwa timu ya Simba SC.

Mjata Mjata ni miongoni mwa mashabiki waliojipatia umaarufu kupitia kipindi cha mashabiki #KipengaXtra cha East Africa Radio na EATV na alipewa jina la utani la #Mpakamafuta, pia alikuwa mwanachama wa EATV Jogging Club.

Kwa taarifa za awali Mazishi ya Mjata yatafanyika Kesho Februari 25, 2025 nyumbani kwao Korogwe Tanga.

Familia ya wafanya biashara wa Mwenge Dar es salaa enao ambalo Mjata Mjata alikuwa anafanyia shughuli zake za kila siku wameandaa utaratibu wa kuchangisha michango ili kufanikisha safari ya kwenda Tanga kwenye mazishi pamoja na kutoa pole kwa familia.

Kwa michango na utaratibu wa kusafiri tuwasiliane na Rajabu Athumani Namba yake ya simu 0678-252728.

Pumzika kwa Amani Mjata Mjata.

Rip pal
 
Back
Top Bottom