Shabiki wa Yanga SC ahamia Simba SC baada ya mwanae kulipiwa fedha za matibabu katika Taasisi ya Moyo ya JKCI

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Baba wa Mtoto Mwamvita ahamia klabu ya Simba SC baada ya mwanae kulipiwa fedha za matibabu katika Simba Week kuelekea Simba day.

Baba mzazi wa mtoto Mwamvita Abdullah aliyepewa msaada wa matibabu wa Shs 2 milioni na Klabu ya Simba katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ameamua kuhama kuishabikia Yanga na kujiunga na miamba hiyo ya Msimbazi.

Mwamvita aliyelazwa hospitalini hapo kwa zaidi ya miezi miwili akisubiri upasuaji, alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kushindwa kupumua vizuri kutokana na kuwa na tundu kwenye moyo amepona na anatarajia kuruhusiwa muda wowote kuanzia sasa.

Baba mzazi wa mtoto huyo, Abdullahi Bakari alisema amehangaika na mtoto huyo kwa takribani miaka mitatu na hivi sasa nashukuru Mungu kwani amepona baada ya kupatiwa matibabu.

"Nashukuru sana kwa dhati Simba, mimi nilikuwa Yanga damu damu, lakini kutokana na kile ambacho Simba wamenifanyia kutoa Shs 2 milioni kumtibia mwanangu nimehama rasmi na sasa nimehamia Simba mimi na familia yangu", alisema Abdullahi.

Naye mtoto Mwamvita alisema anawashukuru wanasimba wote kwa kujitoa kuokoa maisha yake, "Sasa nitaweza kurudi masomoni nashukuru kwa nafasi hii waliyonipa naomba Mungu awaongezee walipopunguza".

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi akielezea Simba News kuwa baada ya kupatiwa fedha za matibabu za mtoto Mwamvita, walimfanyia upasuaji Agosti 24 mwaka huu.

Alisema upasuaji huo ulifuatia baada ya viongozi na wachezaji wa Simba kutembelea taasisi hiyo Agosti 7 mwaka huu katika maadhimisho ya Simba Day na kukutana na Mwamvita ambaye alikuwa akisubiri kufanyiwa upasuaji.

Chanzo: Simba News
 
Ajifunike shuka na mke/mume wake wazae alafu Yanga wajekumtibia/kumtunzia mtoto wake? shame, hata kama ni msaada mbona mwaka 2016 Haji Manara alichangiwa na mashabiki wa Yanga na hakuhama?
Mkuu kama ujapenda vile..! Kumbuka amesaidiwa tu, na si kwa nia ya kumvuta aje pale Msimbazi

Ni vema tu katika kusaidia jamii kwa mambo kama hayo
 
Upoyoyo huo mbona manara tulimchangia na hakuhama? Basi na mrema arudi chama cha zamani ccm maana ndio waliomtibia.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ajifunike shuka na mke/mume wake wazae alafu Yanga wajekumtibia/kumtunzia mtoto wake? shame, hata kama ni msaada mbona mwaka 2016 Haji Manara alichangiwa na mashabiki wa Yanga na hakuhama?
Wewe humjui Haji manara. Alkua Yanga na alichezea yanga kids

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…