Shaffih Dauda mfukuze kazi Baraka Mbolembole

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
23,566
Reaction score
24,891
Nimekuwa msomaji wa habari za michezo katika blogs mbalimbali kama vile ya Shaffih Dauda, Bin Zubeiry, Saleh Jembe, Sports in Bongo nk. Wamiliki wa blogs hii ni wachambuzi na wapiga picha wazuri wa michezo, ninawapongeza kwa kutupasha habari mara kwa mara. Lakini si muda wote wanakuwa wao ndio wanapost habari, bali wanakuwa na baadhi ya waandishi ambao wamepewa sehemu ama kolamu fulani ya kuweka habari katika blogs hizo.

Kule kwa Shaffih Dauda kuna mwandishi mmoja anayeitwa Baraka Mbolembole 'ameajiriwa' katika kolamu inayoitwa 'Jicho la Tatu'. Nimekuwa nikisoma habari zake nakutana na maudhui 'yanayoishambulia' Simba, au kuibeza, au kuitabiria mabaya. Mfano ni usajili wa Mzimbabwe Mwanjale, mwandishi alishambulia sana na kumuita 'kibabu' ambacho hakitaisaidia Simba. Akaja 'kutabiri' kuwa Simba itaambulia sare mechi ya kwanza ya Ruvu Shooting, akaja akatabiri kwamba Simba itachapwa na Azam, akaja akatabiri kwamba Simba itachapwa na Yanga! Pamoja na kufeli kwa tabiri zake zote za nyuma, hachoki kuacha kuitabiria Simba. Utabiri usipotimia atarudi kuponda wachezaji!

Sasa kilichonisukuma hadi kumshauri mmiliki wa blogu hii amfukuze kazi Mbolembole ni hii mechi ya juzi ya Simba na Yanga. Baada ya utabiri wake kushindwa, jana amekuja na jambo la kushangaza kabisa. Si kuhusu goli la Ajibu, wala la Tambwe, wala red card ya Mkude. Jamaa anasema goli la Kichuya la kona iliyoingia moja kwa moja si halali kwa sababu haikutakiwa kuwa kona, bali ilitakiwa mpira uwe wa kurushwa, na kwamba mtoto wa kuokota mpira (ball boy) ndiye aliyeuweka mpira sehemu ya kona, lakini mwamuzi alikuwa ameamuru urushwe! Kwamba Kichuya alitakiwa arushe mpira na wala sio kupiga kona.
Sina hata haja ya kuzungumzia mahali ambapo mpira ulitolewa na beki wa Yanga, maana nikizungumzia nitakuwa kichaa kama mwandishi

Rai yangu ni kumtaka mmiliki wa blogu hii Shaffih Dauda amuondoe mwandishi Baraka Mbolembole katika uandishi kwenye blogu yake kwani anachofanya ni kuishushia hadhi, pengine hata wafadhili wa blog hii wanayaona hayo, na inaweza ikatokea wakajitoa kwa ajili ya habari za uongo

HAPA BEKI WA YANGA ANAUTOA MPIRA, AMBAO MBOLEMBOLE ANADAI UNATAKIWA KUWA WA KURUSHWA




MWAMUZI WA KATI NA WA PEMBENI WOTE WANAASHIRIA KONA




MTOTO ANAYEOKOTA MIPIRA (BALL BOY) ANAYELALAMIKIWA NA MWANDISHI MBOLEMBOLE KUWA ALIFANYA MAKOSA KUUWEKA MPIRA KWENYE KONA
 
Haya malalamiko si ungemtumia Shaffii ,contact zake angalia kwenye hiyo blog uliyosoma
 
Hata JPM analalamikiwa humu humu, wakati physical address ya Ikulu inajulikana! Jiulize nini maana ya JamiiForums: The Home of Great Thinkers
JPM ni Raisi wa Tanzania amechaguliwa atutumikie wananchi na kodi zetu ndio zinamlipa mshahara,kujadili personal blog ya mtangazaji wa radio ndio great thinker?
 
We mbumbumbu unataka waajiliwe wafanyakazi watakaokua wanaisifia simba tu?acha utoto.
 
JPM ni Raisi wa Tanzania amechaguliwa atutumikie wananchi na kodi zetu ndio zinamlipa mshahara,kujadili personal blog ya mtangazaji wa radio ndio great thinker?

Lakini huyo huyo JPM anapiga simu kwenye private media kama sehemu ya kazi zake, sasa sijui kwa nini JF unataka isijadili private blog wakati inachapisha habari for the public!

 
Lakini huyo huyo JPM anapiga simu kwenye private media kama sehemu ya kazi zake, sasa sijui kwa nini JF unataka isijadili private blog wakati inachapisha habari for the public!

Tuna haki ya kumjadili JPM sababu ni kiongozi aliyechaguliwa na wananchi kuongoza Tanzania.Hapo JPM anapiga simu kama msikilizaji/Mtazamaji wa Radio/TV kutoa maoni yake binafsi.

Unacholalamika kipo kwenye blog ya Shaffii na kule ana contact zake na kuna sehemu ya kutoa maoni,mwandikie directly sio kuja kujaza server za JF
 
Hongera mleta mada kwa hoja na ushahidi dhahiri dhidi ya Mbolembole. Ipo dhana kuwa mwandishi huyu ni mpenzi wa Simba aliyeathirika na siasa za kutafuta uongozi ndani ya timu hiyo kwa hiyo ana chuki kuu ambayo bahati mbaya ameshindwa kuitafutia dawa. Badala yake amechanganya chuki na kazi. Kwa kuwa anataka kuwakomoa baadhi ya watu lakini anashindwa kujua kuwa hawatendei haki wengine ambao hawana upande lakini kubwa kuitendea haki fani yake inayomtaka kuwa objective na kuepuka biasness.

Kusema kweli anasikitisha sana maana chuki inaonekana dhahiri ni kama anashindana na watu fulani hivi ndani ya Simba. Siamini kama anafanya kazi kwa faida ya Yanga, ila ana chuki na Simba japo hajatumwa na Yanga.
 
We mbumbumbu unataka waajiliwe wafanyakazi watakaokua wanaisifia simba tu?acha utoto.

Hivi kwa nini kumekuwa na watu wanaojitia ujinga wa kushindwa kujadili hata vitu vya wazi kabisa kama hoja na ushahidi uliotolewa na mleta mda kiasi cha kubezwa? Hivi kuwa na mapenzi na Yanga ni lazima uunge mkono kila kitu cha Yanga au kubeza kila mwenye maoni tofauti? Au kuwa na mapenzi na Simba ni lazima uwe kinyume na kubeza kila mwenye maoni tofauti na Simba? Ina maana kama tunavyojiita familia ya mpira a.k.a watu wa mpira, hatuwezi kujadili kosa la mwamuzi au mchezaji au mwandishi bila kuingiza Usimba na Uyanga?
 
Hata Shafii mwenyewe sio mchambuzi ni shabiki tu kwa hyo hapo wamebalansi moja mikia moja ndala full stop.
 
Mapenzi yanamsukuma vibaya goli la kichuya hutokea mala chache kwa miaka kumi sio tanzania duniani
Toka mayanja wa lyon awafunge azam pale chamazi ishapita hata miezi mitatu? Toka yule mniger wa yanga afunge mapinduzi ushapita hata mwaka? Huyo kichuya mwenyewe sio goli la kwanza sijui itakua imepita miaka 40?
 
Nilifikiri utaleta video kuonyesha mpira ulipotokea tuone wewe na yeye nani muongo na sio chuki tu sbb anawananga lkn kwa picha za mnato hata wewe mnafiki tu manake kwenye hiyo mechi maamuzi ya mipira ya kurusha yalikua tata mara kibao
 
Nilifikiri utaleta video kuonyesha mpira ulipotokea tuone wewe na yeye nani muongo na sio chuki tu sbb anawananga lkn kwa picha za mnato hata wewe mnafiki tu manake kwenye hiyo mechi maamuzi ya mipira ya kurusha yalikua tata mara kibao
Mpira unaotolewa usawa wa eneo la 18 pembeni ya nguzo ya goli huwa unarushwa? Na wewe ni kichaa tu kama huyo Mbolembole
 
Mapenzi yanamsukuma vibaya goli la kichuya hutokea mala chache kwa miaka kumi sio tanzania duniani
Km ulikuja mjini wakati stend ya mkoa ipo ubungo sawa,lkn lile hata kaseja kishafungwa na george nketto pale shamba la bibi
 
Km ulikuja mjini wakati stend ya mkoa ipo ubungo sawa,lkn lile hata kaseja kishafungwa na george nketto pale shamba la bibi
Lakini huyo Kaseja na Nketo wameanza kucheza wakati stendi ya mkoa ipo Ubungo!
 
mi nlidhani unapingana na tathmini zake generally kumbe ni kwasababu anatabiri negative kwa timu yako? anyway mi nadhani labda chambuzi zake ndizo kocha wako huzitumia na kuona mapungufu na kujirekebisha kabla ya mechi.so nadhani ungempongeza kwa kuwa anawashtuaga mapema weaknesses mbalimbali
 
Ni hivi mkuu, jamaa amekuwa anadeal na Simba tu! Angalia makala zake zote, akiitaja Azam basi ujue anazungumzia mechi ya Azam vs Simba, na kadhalika. Lakini hiyo ya kutabiri ilikuwa kwenye utangulizi wa story. Maudhui hasa ya habari hii ni kuhusu madai yake ya jana kwamba kona iliyopigwa na Kichuya haikustahili kuwepo, bali ni mpira wa kurushwa!
 
Me nadhani hata yeye atakua mshabiki kama ulivyokua wewe! Huna haja ya kumuharibia mwezio kibarua chake! kama anaisema simba kila mara na wewe hupendi basi usisome makala zake! Soma hizo blogs nyingine ulizozitaja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…