Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 23,566
- 24,891
Nimekuwa msomaji wa habari za michezo katika blogs mbalimbali kama vile ya Shaffih Dauda, Bin Zubeiry, Saleh Jembe, Sports in Bongo nk. Wamiliki wa blogs hii ni wachambuzi na wapiga picha wazuri wa michezo, ninawapongeza kwa kutupasha habari mara kwa mara. Lakini si muda wote wanakuwa wao ndio wanapost habari, bali wanakuwa na baadhi ya waandishi ambao wamepewa sehemu ama kolamu fulani ya kuweka habari katika blogs hizo.
Kule kwa Shaffih Dauda kuna mwandishi mmoja anayeitwa Baraka Mbolembole 'ameajiriwa' katika kolamu inayoitwa 'Jicho la Tatu'. Nimekuwa nikisoma habari zake nakutana na maudhui 'yanayoishambulia' Simba, au kuibeza, au kuitabiria mabaya. Mfano ni usajili wa Mzimbabwe Mwanjale, mwandishi alishambulia sana na kumuita 'kibabu' ambacho hakitaisaidia Simba. Akaja 'kutabiri' kuwa Simba itaambulia sare mechi ya kwanza ya Ruvu Shooting, akaja akatabiri kwamba Simba itachapwa na Azam, akaja akatabiri kwamba Simba itachapwa na Yanga! Pamoja na kufeli kwa tabiri zake zote za nyuma, hachoki kuacha kuitabiria Simba. Utabiri usipotimia atarudi kuponda wachezaji!
Sasa kilichonisukuma hadi kumshauri mmiliki wa blogu hii amfukuze kazi Mbolembole ni hii mechi ya juzi ya Simba na Yanga. Baada ya utabiri wake kushindwa, jana amekuja na jambo la kushangaza kabisa. Si kuhusu goli la Ajibu, wala la Tambwe, wala red card ya Mkude. Jamaa anasema goli la Kichuya la kona iliyoingia moja kwa moja si halali kwa sababu haikutakiwa kuwa kona, bali ilitakiwa mpira uwe wa kurushwa, na kwamba mtoto wa kuokota mpira (ball boy) ndiye aliyeuweka mpira sehemu ya kona, lakini mwamuzi alikuwa ameamuru urushwe! Kwamba Kichuya alitakiwa arushe mpira na wala sio kupiga kona.
Sina hata haja ya kuzungumzia mahali ambapo mpira ulitolewa na beki wa Yanga, maana nikizungumzia nitakuwa kichaa kama mwandishi
Rai yangu ni kumtaka mmiliki wa blogu hii Shaffih Dauda amuondoe mwandishi Baraka Mbolembole katika uandishi kwenye blogu yake kwani anachofanya ni kuishushia hadhi, pengine hata wafadhili wa blog hii wanayaona hayo, na inaweza ikatokea wakajitoa kwa ajili ya habari za uongo
HAPA BEKI WA YANGA ANAUTOA MPIRA, AMBAO MBOLEMBOLE ANADAI UNATAKIWA KUWA WA KURUSHWA
MWAMUZI WA KATI NA WA PEMBENI WOTE WANAASHIRIA KONA
MTOTO ANAYEOKOTA MIPIRA (BALL BOY) ANAYELALAMIKIWA NA MWANDISHI MBOLEMBOLE KUWA ALIFANYA MAKOSA KUUWEKA MPIRA KWENYE KONA