Sasa hapo mkuu ni wapi shaffih kamuattack Babra kwa maelezo yake anazungumzia mtu mwenye nafasi ya CEO ndani ya simba kushindwa kutimiza majukumu yake kwa wakati na ni ushauri mzurii hata sisi wanasimba kwa tulipofikia hatufurahii kuhangaika na wachezaji wetu tena tegemeo wakiwa wamebakisha miezi miwili mkataba uishe hizi ni presha za kujitakia ili baadae tumlaumu mchezaji hana mapenzi na timu wakati sote tunajua hawa vijana mpira ndio kazi yao ni zaidi ya mapenzi na ushabiki.
Kwaio dauda ndio anaepima utendaji wa CEO wa Simbasc?!! Vitu vingine hao mnaowaita wachambuzi ni wapuuzi tu!!
Mamlaka ya kupima utendaji wa Simbasc ni bodi ya wakurugenzi ya Simba!!yenyewe ndio imempaka terms and conditions za kazi yake, yeye anafanya kazi kwa maelekezo ya bodi ya club.
Suala la mikataba ya wachezaji yeye analiwasilisha kwenye bodi,na bodi ndio inampa maelekezo CEO baada ya kupata ushauli toka kwenye benchi la ufundi!!
Uyo dauda kwa akili zake za kizamani anafikili kuwa CEO anaamua tu kumuongeza mchezaji mkataba kisa tu mchezaji mwandamizi!!
Kuhusu Simbasc kufanya press ni kutokana na matukio husika, Simbasc imekuwa inashiriki clubs champion,na matukio mengi ya umuhimu kuhusu mashindano na taarifa za club, ivyo hakuna kosa kuitisha press kujulisha umma kila kinachojili,maana si watu wote wanafuatilia mitandao ya club.
Mwisho kufananisha utendaji wa CEO wa taasisi moja na nyingine kiutendaji ni ujinga na kujipendekeza,kila taasisi ina mifumo yake na malengo yake,ni kama vile mtu ufananishe utendaji kazi wa Uhuru Kenyata,na Hayati Magufuli,kila mtu ana maono yake na mitizamo yake katika uendeshaji wa mambo.
Wachambuzi wengi wapunguze miemko wajaribu kutafuta habari na kubalance habari wasiwe wanajifanya kila kitu wanajua na wako sahihi.