Shafii Dauda anafaa kuadhibiwa kwa uchochezi

Mkude alimdondosha mwamuzi kwa kumpuga mtama, then mwamuzi aliposimama akamlima red card, baada ya siku tatu kamati ya 'wahuni' inakaa na kuifuta red card na kumpa kalipio mwaluzi, tena bila hata kusoma report ya mechi ile......
Na bado mkileta fyongo kamati zetu za wahuni tutazidi kuwahunisha zaidi
 
Shafii dauda sio mchambuzi ni mchambuzi uchwara nliachaga kumsikilizaga zamani sana, azam ndo kuna wachambuzi akina Jeff Lea, Ali mayai. ile video jana nmeiona vizur kwenye kipindi cha kipyenga cha mwisho cha osman kazi wameirudia ile video zaidi ya mara kumi yule mwamuzi hajaguswa hajasukumwa na wala hajategwa, osman kazi mwenye amesema ile haikua hata yellow card sababu mwamuzi hajaguswa, na mkude alikua na haki ya kusikilizwa sababu yeye ndo captain, shafii boya sana
Mahaba yakizidi yanatoa ufahamu wewe uliona video ambayo pengine imeeditiwa tuliokuwa uwanjani tuliona Mkude akimsukuma mwamuzi tena sio mara moja na ndiyo maana mashabiki wengi wlioona tukio wanamlaumu Mkude kuwa ni Yanga na alifanya vile ili apewe kadi nyekundu.
 
Duh,huu ndo mpira wa Tanzania watu wanachangishana mamilioni kwa ajili ya mechi moja tu. Hizi Simba na Yanga ili tupate maendeleo ya soka ni mpaka zife au zishuke daraja kwa muda mrefu ndipo tutakapoamka huu usingizi wa pono!!
Ama kweli Tanzania tumerogwa kabisa si bure!!!
khaaa....wamekulazimisha wewe kuchanga?
 
Mahaba yakizidi yanatoa ufahamu wewe uliona video ambayo pengine imeeditiwa tuliokuwa uwanjani tuliona Mkude akimsukuma mwamuzi tena sio mara moja na ndiyo maana mashabiki wengi wlioona tukio wanamlaumu Mkude kuwa ni Yanga na alifanya vile ili apewe kadi nyekundu.
mkude hakumsukuma mwamuzi ...alijikwaa...kama unasema video ime editiwa hebu wewe leta ambayo haijaeditiwa
 
Tuwe wakweli. TFF na Kamati zake ina udhaifu mkubwa katika kusimamia Ligi Kuu hapa nchini. Wenye makengeza nimekuwa nikiwasikia wakilalama kwamba TFF na Kamati zake inaibeba Yanga. Nashangaa. Hakuhitajiki hata miwani ya plastiki kibaini kwamba:
1. Maamuzi ya TFF na kamati zake ni ya kuabudu Timu tatu kubwa za Dar kwa kuziridhia matakwa yao hata kama ni kinyume na Sheria, kanuni na taratibu zinazotawala mpira wa miguu hapa nchini. Pale mmoja wapo anapobebwa, ndiyo wenzake wawili na washabiki wao ndio hulalamika kwamba mwenzao amebebwa.
2. Anayebisha kwamba Azam haibebwi aseme ruhusa ya kuacha Ligi Kuu na kwenda kucheza bonanza nje ya nchi huku akiwalazimishia wenzake viporo ni nini.
3. Anayebisha kwamba Yanga habebwi aseme nini maana ya hukumu ya Ngoma kumpiga kiwiko mchezaji wa Simba kwenye Ligi ya Msimu uliopita kutotolewa mpaka leo, na imeishia wapi.
4. Anayesema kwamba Simba haibebwi atueleze ilikuwaje kanuni ya mchezaji kuchagua mechi ya kuikosa baada ya kuoneshwa kadi nyekundu ikatumika kabla ya kutangazwa na kuinufaisha Simba pekee, baada ya hapo mlango ukafungwa kwa komeo la chuma na ufunguo ukatoswa baharini. Au aeleze utamaduni wa kufuta kadi bila ya mhusika kuilalamikia umeanza lini hadi hii ya Mkude ikawa angalau ya pili.
Najua kuna wanaonishangaa sizungumzii magoli yanayolalamikiwa na Simba dhidi ya Yanga, lakini mwenye akili ya tafakuri hawezi kulihusisha hilo moja kwa moja na TFF na Kamati zake. Maana hata tukijaalia kuwa ni kweli waamuzi waliboronga kwa makusudi, huo kisheria ni ukorofi wao na si wa TFF na Kamati zake. Lakini anayenufaika na maamuzi yanayoaminika kuwa ni ya kiushikaji siyo Yanga peke yake. Ndio maana hata kwenye mechi hiyohiyo, Yanga nao wanalalamika kwamba mwamuzi aliliweka kwenye mizani pambano hilo mara tu baada ya nyekundu ya Mkude. Julio naye anawalalamikia waamuzi kwa kufungwa na Mbeya City. Na kadhalika. Ni dhambi kupuuza malalamiko ya timu nyengine dhidi ya waamuzi wanapocheza na isiyo Yanga, kwa sababu tu wao ni timu ndogo. Ama tuyape uzito malalamiko ya timu zote dhidi ya marefa uzito sawa na ya Simba dhidi ya Yanga, au yote tuyatupilie mbali.
Nionavyo, majigambo ya kijinga ya viongozi, wachezaji na wapenzi kabla ya michezo yao ndiyo chanzo kikuu cha dhana hii potofu ya timu kubebwa na TFF ilhali hata kama madai ya ubebaji yakithibitika bado hayatoshi kuhitimisha kwamba yamefanywa na TFF na kamati zake. Kusingizia marefa ni mbinu ovu ya wanamajigambo hawa kutawala kushindwa (defeat management) kwao kwenye mechi waliyotangulia kuisema kwamba ' tutashinda kwa hali yoyote, tutawafunga watake wasitake, wapenzi wasiwe na hofu, hakuna timu ya kutufunga, nani kama timu yetu?, wao ni wateja wetu tu, tuna uhakika wa pointi tatu' n.k. Msemaji wa timu hiyo anapoambulia kipigo ama sare huishia kutafuta kisingizio ili asihojiwe kushindwa kwa majigambo yake. Ndio maana makocha wasio tabia hii huwasikii kulalamika hivyo. Kocha wa Burnley hakujigamba kwamba lazima angeifunga Arsenal ndio maana walipofungwa goli linaloweza kuwa kweli la mkono hawakun'goa viti uwanjani.
Ni upuuzi kudhani mechi zetu kuchezeshwa na marefa wa nje ndio kutaondoa ghasia za aina hii viwanjani, kama kudhani kwamba tunahitaji wageni kuongoza Kamati zetu za Uchaguzi ndio malalamiko ya kuibiwa kura yataondoka. Tunachohitaji ni wadau wa timu zetu kujitambua, na kwamba kufungwa siyo lazima maana yake iwe ni ubovu wa timu, na kwamba hakuna timu isiyofungwa, na kwamba waamuzi ni wanadamu na kwa hivyo kukosea kwao ni lazima, na kwamba hakuna namna ya kubadilisha maamuzi ya refa ukiwa ndani au nje ya uwanja, na kwamba mpira haujafikia uadilifu wa kuwa kila anayestahiki ndiye anayefanikiwa kwa mujibu wa anavyostahiki, na kwamba wachezaji nao ni wanadamu na kwa hivyo lazima watakosea mara nyengine hata kusababisha timu kufungwa, na kwamba mpira ni mchezo wa kistaarabu usiohitaji hasira.
Ukweli mtupu.Anayebisha ni ......
 
Kwani kati ya wachambuzi wa michezo shafii naye yupo.

Shaffii ni mchambuzi wa Udaku na umbea. Si alikosa kazi tff afu yy ni shabiki wa Yanga.

Ndio maana huwa sisikilizi cloids media maisha yangu yote. Coz hawanaga habari.
 
Hebu tuvue viatu vya uSimba ama UYanga na baadaye tuvae vya mwamuzi Saaya. Umezungukwa na wachezaji wenye hasira huku wakikusukimasukuma. Mmoja aliye nyuma yako anajikwaa kwa mwenzake na katika kupepesuka kwake akakuangusha bila ya yeye kuanguka. Hayo yote yanatokea ndani ya sekunde chache. Akili yako itafikiriaje kama si kwamba amekuangusha kwa makusudi? Na kwa maamuzi hayo atakuwa amekosea? Kamati ilipaswa kuangalia mazingira ya mwamuzi kutoa kadi ile. Kamati iliangalia video kwanza kabla ya kuamua kwa sababu walikuwa na muda wa kufanya hivyo. Ingekuwa sahihi Kamati kuifuta kadi hiyo kama na mwamuzi naye alikuwa na muda wa kuangalia video ndipo atoe hukumu!
 
Nilishangaa juzi Julio kustaafu mpira kwa ubabaishaji wa waamuzi,hapa sio waamuzi tu shida iko pale TFF
Ngoja niendelee kufurahia maisha mwaka wa nne sasa sishabikii kitu kinachoitwa mpira wa Tanzania hata timu ya Taifa.....maana niliona napata stress zisizo na maana bila sababu.....eti Simba mara Yanga....siku hizi si kuna Azamu...ni ujinga mtupu!!!
Hahaha mkuu Tanzania hatuna mpira tuna Kabumbu.
 
Huyu jamaa ni waajabu sana sana, anajifanya anajua sana mambo ya soka wakati hajui kitu, hata uongozi wa tff asidhani ni kiki ya kuupata
 
Mkude alimdondosha mwamuzi kwa kumpuga mtama, then mwamuzi aliposimama akamlima red card, baada ya siku tatu kamati ya 'wahuni' inakaa na kuifuta red card na kumpa kalipio mwaluzi, tena bila hata kusoma report ya mechi ile......

Ajib naye anafunga goli zuri lakini ghafla kundi la wahuni wawili wanalikataa na kusema mfungaji aliotea.....
Nayo kamati ya wahuni inakaa bila kusema chochote kuhusu hilo hata bila ya kusoma ripoti ya mechi ile...
 
Nilidhani hushughuliki tena na VPL, na kwamba hizo habari za Julio umeziona huko kwenye Ligi unayoishughulikia ambayo ndio sijui kama ni EPL au La Liga mkuu!
Ha ha ha ha mkuu habari za Julio si nilisikia kwenye taarifa kama habari zingine!!?? Ila we umefanya uchochezi milioni saba itakuhusu
 
Tuwe wakweli. TFF na Kamati zake ina udhaifu mkubwa katika kusimamia Ligi Kuu hapa nchini. Wenye makengeza nimekuwa nikiwasikia wakilalama kwamba TFF na Kamati zake inaibeba Yanga. Nashangaa. Hakuhitajiki hata miwani ya plastiki kibaini kwamba:
1. Maamuzi ya TFF na kamati zake ni ya kuabudu Timu tatu kubwa za Dar kwa kuziridhia matakwa yao hata kama ni kinyume na Sheria, kanuni na taratibu zinazotawala mpira wa miguu hapa nchini. Pale mmoja wapo anapobebwa, ndiyo wenzake wawili na washabiki wao ndio hulalamika kwamba mwenzao amebebwa.
2. Anayebisha kwamba Azam haibebwi aseme ruhusa ya kuacha Ligi Kuu na kwenda kucheza bonanza nje ya nchi huku akiwalazimishia wenzake viporo ni nini.
3. Anayebisha kwamba Yanga habebwi aseme nini maana ya hukumu ya Ngoma kumpiga kiwiko mchezaji wa Simba kwenye Ligi ya Msimu uliopita kutotolewa mpaka leo, na imeishia wapi.
4. Anayesema kwamba Simba haibebwi atueleze ilikuwaje kanuni ya mchezaji kuchagua mechi ya kuikosa baada ya kuoneshwa kadi nyekundu ikatumika kabla ya kutangazwa na kuinufaisha Simba pekee, baada ya hapo mlango ukafungwa kwa komeo la chuma na ufunguo ukatoswa baharini. Au aeleze utamaduni wa kufuta kadi bila ya mhusika kuilalamikia umeanza lini hadi hii ya Mkude ikawa angalau ya pili.
Najua kuna wanaonishangaa sizungumzii magoli yanayolalamikiwa na Simba dhidi ya Yanga, lakini mwenye akili ya tafakuri hawezi kulihusisha hilo moja kwa moja na TFF na Kamati zake. Maana hata tukijaalia kuwa ni kweli waamuzi waliboronga kwa makusudi, huo kisheria ni ukorofi wao na si wa TFF na Kamati zake. Lakini anayenufaika na maamuzi yanayoaminika kuwa ni ya kiushikaji siyo Yanga peke yake. Ndio maana hata kwenye mechi hiyohiyo, Yanga nao wanalalamika kwamba mwamuzi aliliweka kwenye mizani pambano hilo mara tu baada ya nyekundu ya Mkude. Julio naye anawalalamikia waamuzi kwa kufungwa na Mbeya City. Na kadhalika. Ni dhambi kupuuza malalamiko ya timu nyengine dhidi ya waamuzi wanapocheza na isiyo Yanga, kwa sababu tu wao ni timu ndogo. Ama tuyape uzito malalamiko ya timu zote dhidi ya marefa uzito sawa na ya Simba dhidi ya Yanga, au yote tuyatupilie mbali.
Nionavyo, majigambo ya kijinga ya viongozi, wachezaji na wapenzi kabla ya michezo yao ndiyo chanzo kikuu cha dhana hii potofu ya timu kubebwa na TFF ilhali hata kama madai ya ubebaji yakithibitika bado hayatoshi kuhitimisha kwamba yamefanywa na TFF na kamati zake. Kusingizia marefa ni mbinu ovu ya wanamajigambo hawa kutawala kushindwa (defeat management) kwao kwenye mechi waliyotangulia kuisema kwamba ' tutashinda kwa hali yoyote, tutawafunga watake wasitake, wapenzi wasiwe na hofu, hakuna timu ya kutufunga, nani kama timu yetu?, wao ni wateja wetu tu, tuna uhakika wa pointi tatu' n.k. Msemaji wa timu hiyo anapoambulia kipigo ama sare huishia kutafuta kisingizio ili asihojiwe kushindwa kwa majigambo yake. Ndio maana makocha wasio tabia hii huwasikii kulalamika hivyo. Kocha wa Burnley hakujigamba kwamba lazima angeifunga Arsenal ndio maana walipofungwa goli linaloweza kuwa kweli la mkono hawakun'goa viti uwanjani.
Ni upuuzi kudhani mechi zetu kuchezeshwa na marefa wa nje ndio kutaondoa ghasia za aina hii viwanjani, kama kudhani kwamba tunahitaji wageni kuongoza Kamati zetu za Uchaguzi ndio malalamiko ya kuibiwa kura yataondoka. Tunachohitaji ni wadau wa timu zetu kujitambua, na kwamba kufungwa siyo lazima maana yake iwe ni ubovu wa timu, na kwamba hakuna timu isiyofungwa, na kwamba waamuzi ni wanadamu na kwa hivyo kukosea kwao ni lazima, na kwamba hakuna namna ya kubadilisha maamuzi ya refa ukiwa ndani au nje ya uwanja, na kwamba mpira haujafikia uadilifu wa kuwa kila anayestahiki ndiye anayefanikiwa kwa mujibu wa anavyostahiki, na kwamba wachezaji nao ni wanadamu na kwa hivyo lazima watakosea mara nyengine hata kusababisha timu kufungwa, na kwamba mpira ni mchezo wa kistaarabu usiohitaji hasira.
comment nzuri sana [emoji122] [emoji122]
 
Back
Top Bottom