Mapato zaidi yanatoka wapi sasa kma sio lazima kila mtu kwenda kiwanjani.??
Azam wanasema wakicheza na YANGA ama SIMBA pale TAIFA mara mbili mbili kwa msimu, inamaanisha wamecheza big match zote UGENINI, wanakosa ile HOME ADVANTAGE
Huyu Bwana anashindwa kujitambua kabisa na ni mpotoshaji maana sababu ya mechi za Azam na Simba na Yanga kuchezwa Taifa ni za kiusalama zaidi ukizingatia uwanja wa Azam Complex ni mdogo sana ku accommodate mashabiki wa hizi timu kubwa mbili na hili linatokana na kuwa uwanja huo hupo hapa Dar eneo ambalo hizi timu zina mashabiki maelfu watakaoweza kwenda pale Chamazi lakini pia uwanja wa Taifa stil ni neutral ground kwa timu zote maana haumilikiwi na Simba wala Yanga na Azam pia ni timu ya Dar es salaam tena kijiografia inatoka wilaya ya Temeke ambapo uwanja wa Taifa upo.
Huyu Bwana anataka mechi ichezwe Chamazi yatokee maafa ndio ajue ni hatari lakini pia ata Hoja ya mapato nayo ni ya msingi timu zetu zinahitaji fedha kwa wingiza mlangoni kama kuna opportunity hiyo uwanja wa Taifa kwa nini wasiitumie.
Maafa gani nyie..? Ni mpangilio tu unakosekana na watu hasa wa tff na makomandoo wa simba/yanga kutaka kujipatia pesa kupitia mechi hizi. Uwanja wa united pale OT unachukua watu takribani 77,000 na uwanja kama turf moor unachukua watu wasiozidi 25,000 lakini bado united inaenda kucheza pale,mbona hatujawahi kusikia maafa?
Pale Misri viwanja vyao ni vikubwa lakini maafa almost daily na nyie ni mashaidi.
Note: watu kuleta fujo na kusababisha maafa haijalishi uwanja ni mkubwa au mdogo
Mimi nadhani hujasoma vizuri hoja zangu umekimbilia kujibu tu halafu sidhani kama mifano ya uingeleza ina suit mazingira kuanzia usalama mpaka miundo mbinu pitia vizuri nilichokijibu ndio urudi uandike upya.