"Yanga SC, imesajili wachezaji wengi sana ila ni waviwango vya chini sana na bei poa tofauti na Simba SC, ambayo pengine imetumia pesa mara Tatu zaidi ya pesa ambazo Yanga wametumia.
"Yanga Inaweza kuwa bora ikiwa hawa wachezaji watatokea wachezaji bora na majina kuwa makubwa ila hadi sasa wako kawaida sana ni 50% kufanya poa wakati huo Simba yenye mastaa kubao pia Inaweza fanya vibaya ila Simba SC, ni 90% kufanya vizuri kulinga na uwekezaji wao wa pesa nyingi kuliko klabo yeyote Tanzania na Africa Mashariki.
Na ukinipinga kuhusu usajili wa Simba SC kuwa ndio sajili ya pesa nyingi kuliko klabu yeyote kanda hii wewe hujui mpira" - Shaffh Dauda
Maoni yangu: unapozungumza/kutoa maoni yako bila fact ni sawa na kufurahisha genge la wanywa pombe au kahawa tu.
Kusema kuwa Simba SC wametumia pesa nyingi kuliko Yanga SC katika usajili ilikupasa kuweka evidence ya mikataba ya wachezaji ili tuwe sawa lakini kutoa maneno matupu hauna tofauti na mshehereshaji katika vilinge vya kahawa.
Kuzungumza kwamba wachezaji wa Yanga SC uwezo wao ni wa kawaida he umewapima kwa kipi?
Na kusema kuwa wachezaji wa Simba SC wanauwezo mkubwa kwa asilimia 90% umeangalia kwa lipi?
Hupaswi kuzungumza tu ulipaswa kuchambua kila engo na kutofautisha huo ubora unaousema lakini tofauti na kufanya hivyo ni Bora unge kaa kimya tu kuliko kulazimisha watu/mashabiki wakubaliane na wewe.
NALIA NGWENA nakujibu na ninakuambia kuwa wewe ndiyo hujui mpira na tukitoa wachambuzi Bora kumi katika hii nchi wewe haumo kabisa.
Kipindi kile ulikua unasoma habari za huko unakuja kuwasimulia kwenye redio watu wanakuona unajua sana lakini hivi Sasa mambo yapo wazi sana huwezi kumdanganya mtu.