Shahidi kesi ya Zumaridi asahaulika gerezani asababisha kesi yashindwa kusikilizwa Mahakamani

Shahidi kesi ya Zumaridi asahaulika gerezani asababisha kesi yashindwa kusikilizwa Mahakamani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kesi namba 10 inyomkabili Diana Bundala Maarufu kama mfalme Zumaridi na wafuasi wake 8 imeshindwa kuendelea Oktoba 31, 2022 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza kutokana na Shahidi namba sita ambae pia ni mshtakiwa katika kesi hiyo, Suzana Simon kutoletwa Mahakamani hapo.

Zumaridi na wafuasi wake wanakabiliwa na kesi ya kuwazuia maafisa wa serikali kutekeleza majukumu yao na kuwajeruhi Askari Polisi.

Wakili wa utetezi Linus Amri ameiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine ya kusikiliza shauri hilo kwani wasingeweza kujitetea bila idadi ya washtakiwa kutimia.

Aidha, katika shauri namba 11 linalomkabili Zumaridi dhidi ya Jamhuri, wakili wa upande wa Jamhuri Martha Mwadenya ameomba kupangwa tarehe nyingine kwani upelelezi bado haujakamilika katika shauri hilo.

Baada ya wakili huyo kudai upelelezi bado haujakamilia Hakimu mkazi mwandamizi Boniventure Lema ameiahirisha kesi hiyo hadi tarehe 14 Novemba 2022 itakapotajwa tena.

Chanzo: EATV
 
Zumaridi amepaniwa kufungwa kesi hii.

Ajiandae kisaikolojia
 
Amegeuziwa kesi kwamba yeye ndio aliwajeruhi mapolisi, Katiba mpya ni muhimu sana
 
Back
Top Bottom