Boss la DP World
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 2,318
- 8,464
Mlikubali wenyewe, bila mtutu kichwani,
Mkaazimu nipewe, kwa udi na kwa ubani,
Akasaini mwenyewe, kwa agizo la fulani,
Kama hamtaki ndoa, rudisheni pesa zangu.
Aliyeleta mzozo, ni mtoto mtukutu,
Akavujisha uozo, ukafika hadi Mbutu,
Wakatilia mkazo, wananzengo wenye utu,
Kama hamtaki ndoa, rudisheni pesa zangu.
Mimi boss la DP, sina kinyongo rohoni,
Hata UNDP, nao wananitamani,
Similiki tu DP, nina midege angani,