Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,319
WIZARA ZIMEWASHINDA
!
Waziri Mkuu Pinda, metuacha na kololo!
Aonesha bado kinda, bado amelala dolo!
Kuongoza amepinda, liko wapi atendalo?
Wizara zimewashinda
Ninakuomba Mkubwa, naomba unisikie
Umuondoe Kawambwa, Elimu simpangie
Umempa kazi kubwa, ameshindwa nikwambie
Wizara zimewashinda
Nako wizara ya Maji, tunachokunywa matope!
Matope hawayachuji, tupate maji meupe!
Na huko kwenye vijiji, Maghembe kawa mapepe!
Wizara zimewashinda
Kilimo ndiyo kabisa, kwa kweli wamekiviza
Mawaziri watutusa, wakulima wawaliza!
Si kilimo cha kisasa, akifanyacho Chiiza!
Wizara zimewashinda
Nayo wizara ya Fedha, uchumi watelekeza!
Mgimwa kakosa radha, haongozi anacheza!
Nchi inataka kadha, kadha wa kadha ni giza!
Wizara zimewashinda
Rejea kwenye Nishati, wafanyalo hatuoni!
Si hayati si mamati, wanatuweka kizani!
Na TANESCO maiti, itajafufuka lini?
Wizara zimewashinda
Nako huko TAMISEMI, miji mekuwa mizigo?
Kutwa kuchonga ulimi, ufanisi ni mdogo!
Hawa Ghasia hasemi, wizara kwenda upogo!
Wizara zimewashinda
Turudi kwenye Michezo, Habari Utamaduni
Huku nako ni uwozo, maendeleo sioni!
Tunaomba muongozo, kinachokwamisha nini?
Wizara zimewashinda
Na wizara ya watoto, Simba sasa kawa Swala?
Mpambana na mazito, leo mtu wa kulala!
Kama niko kwenye ndoto, sijaamini Bwakila!
Wizara zimewashinda
Hizo nyingine wizara, Mkubwa unazijuwa!
Ni chache zenye ubora, zingine zasuwasuwa!
Fanya kukurukakara, mambo uyaweke sawa
Wizara zimewashinda
Wanakwenda msagunda, Mkubwa unawalinda?
Ndege mpasua sanda, analia tutashinda?
Nchi iko njia panda, hatujajua pa kwenda!
Wizara zimewashinda
Mussa Ally Salum Bwakila,
Mussa_ally@ymail.com
https://www.facebook.com/mussa.allybwakila?hc_location=stream