Wameyataka wenyewe,
Wameingia kiwewe,
Wanahaha kama mwewe,
Haya hawakuyajua
Majigambo yameisha,
Kura hazikuwatosha,
Wameijua Arusha,
Kwamba si ya kuchezea
Walifikiri mabomu,
Yangefifisha fahamu,
Za watu wenye elimu,
Elimu ya uraia
Elimu ya ufahamu,
Kwamba hii sisiemu,
Ni ya watu wadhalimu,
Watu wameigundua
Watu wasio huruma,
Na tena wenye dhuluma,
Polisi wanawatuma,
Uhai wanatutoa
Wamechoka kuongoza,
Mizengo alitangaza,
Yule mwana wa Kayanza,
Na sisi tulisikia
Kwamba hana mbadala,
Wa wao kututawala,
Bali ni vyombo vya dola,
Ndivyo wanajivunia
Hakika wameumbuka,
Na jasho limewatoka,
Aibu imewafika,
Aibu ya historia
Na hizo siasa zao,
Za "wapigeni tu hao",
Hazitawafaa wao,
BALI WATAANGAMIA