Shairi maalumu kwa Mwigulu Nchemba

Shairi maalumu kwa Mwigulu Nchemba

Nadhan huyu mwandishi ni kijana wangu wa chuo cha mipango anatokea Kigoma ndio mtaalam wa hizi mambo naona hata mahadhi ya zile tungo zake ,fano wa ile aliyowahi kumpongeza kamanda mnyika pale dodoma kwenye mkutano wa cdm baada ya kutoa ile hoja ya maji na kupigwa chini
 
Wameyataka wenyewe,
Wameingia kiwewe,
Wanahaha kama mwewe,
Haya hawakuyajua

Majigambo yameisha,
Kura hazikuwatosha,
Wameijua Arusha,
Kwamba si ya kuchezea

Walifikiri mabomu,
Yangefifisha fahamu,
Za watu wenye elimu,
Elimu ya uraia

Elimu ya ufahamu,
Kwamba hii sisiemu,
Ni ya watu wadhalimu,
Watu wameigundua

Watu wasio huruma,
Na tena wenye dhuluma,
Polisi wanawatuma,
Uhai wanatutoa

Wamechoka kuongoza,
Mizengo alitangaza,
Yule mwana wa Kayanza,
Na sisi tulisikia

Kwamba hana mbadala,
Wa wao kututawala,
Bali ni vyombo vya dola,
Ndivyo wanajivunia

Hakika wameumbuka,
Na jasho limewatoka,
Aibu imewafika,
Aibu ya historia

Na hizo siasa zao,
Za "wapigeni tu hao",
Hazitawafaa wao,
BALI WATAANGAMIA
 
Shairi nzuri xana,umejaribu kuigiza jinsi ya kuandika utenzi hongera umejitahidi japo beti nne za mwanzo umejaribu kufananisha vina na baadhi kufwata mzani.
yote hyo ikiwa nikuwasilisha hisia zako.
km jamii ya watanzania ni vema kufanya utafiti wa kina zaidi ili kuweka jambo fulani bayani.
Nimaoni yangu kwako kwakuwa utenzi ni tajiri xana wa tamathali za semi sijaona haja ya ww kutumia moja kwa moja jina la msh NCHEMBA.
ni bora ungetumia majina ya miti,wanyama au tabia.
kwa mantiki hiyo shairi lako liko UCHI ni vema siku nyingine uvishe NGUO kwa usalama wako na amani ya nchi yetu.
 
Wameyataka wenyewe,
Wameingia kiwewe,
Wanahaha kama mwewe,
Haya hawakuyajua

Majigambo yameisha,




Kura hazikuwatosha,
Wameijua Arusha,
Kwamba si ya kuchezea

Walifikiri mabomu,
Yangefifisha fahamu,
Za watu wenye elimu,
Elimu ya uraia

Elimu ya ufahamu,
Kwamba hii sisiemu,
Ni ya watu wadhalimu,
Watu wameigundua

Watu wasio huruma,
Na tena wenye dhuluma,
Polisi wanawatuma,
Uhai wanatutoa

Wamechoka kuongoza,
Mizengo alitangaza,
Yule mwana wa Kayanza,
Na sisi tulisikia

Kwamba hana mbadala,
Wa wao kututawala,
Bali ni vyombo vya dola,
Ndivyo wanajivunia

Hakika wameumbuka,
Na jasho limewatoka,
Aibu imewafika,
Aibu ya historia

Na hizo siasa zao,
Za "wapigeni tu hao",
Hazitawafaa wao,
BALI WATAANGAMIA

hakika unastahili pongezi kwa mashairi yako nadhimu hongera tuonane 2015
 
سشبه سشىش ةصهلعمع ىؤاثةﻻش ىه ةسثىلث
 
mhh haya maneno jamani kwani Mwigulu kawafanya nini hata kumsema hivi! hamkutaka atetee chama chake? mbona nyie mnatetea chama chenu?
 
Back
Top Bottom