Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwigulu punguza spidi mkuu kunawatu unafanya wasilale kabisa.
Kunawatu wengine watakufa mapema san mtu kutwa anamwaza mwanaume mwenzake pole mkuu.
4-0. M4C inachanja mbuga,Mwigulu punguza spidi mkuu kunawatu unafanya wasilale kabisa.
Wameyataka wenyewe,
Wameingia kiwewe,
Wanahaha kama mwewe,
Haya hawakuyajua
Majigambo yameisha,
Kura hazikuwatosha,
Wameijua Arusha,
Kwamba si ya kuchezea
Walifikiri mabomu,
Yangefifisha fahamu,
Za watu wenye elimu,
Elimu ya uraia
Elimu ya ufahamu,
Kwamba hii sisiemu,
Ni ya watu wadhalimu,
Watu wameigundua
Watu wasio huruma,
Na tena wenye dhuluma,
Polisi wanawatuma,
Uhai wanatutoa
Wamechoka kuongoza,
Mizengo alitangaza,
Yule mwana wa Kayanza,
Na sisi tulisikia
Kwamba hana mbadala,
Wa wao kututawala,
Bali ni vyombo vya dola,
Ndivyo wanajivunia
Hakika wameumbuka,
Na jasho limewatoka,
Aibu imewafika,
Aibu ya historia
Na hizo siasa zao,
Za "wapigeni tu hao",
Hazitawafaa wao,
BALI WATAANGAMIA
Kunawatu wengine watakufa mapema san mtu kutwa anamwaza mwanaume mwenzake pole mkuu.