SHAIRI: Najipa Moyo

SHAIRI: Najipa Moyo

ramadhani kimweri

Senior Member
Joined
Apr 22, 2016
Posts
181
Reaction score
179
NAJIPA MOYO.
Matatizo niliyo nayo, kuyabeba ni michosho
Lakini hali iwayo, naloa maji ya jasho
Bado ninajipa moyo, kuwa nitapata kesho.

Ninapotazama mbele, giza nene naliona
Lini nitafika kule, moyo tumaini sina
Hata nipige kelele, kila siku kama jana.

Shibe yangu ni njaa, na maji nimeze mate
Naonekana kichaa, natafuta nisipate
Natembea natambaa, niende nijikokote..

Ya jana ndio ya leo, sionagi tofauti
Mie sina kimbilio, na wala sifurukuti
Maisha yangu kilio, kila siku yalaiti..

Ukitegemea waja, ipo siku utalia
Niliposhikwa na haja, wote wakaniambia
Nakuniona kioja, nataabika dunia.

Tumaini langu moja, ndio nalitegemea
Ajuae zangu haja, kwake nimeegemea
Ni yeye mola mmoja, haya kuniondolea.

[emoji2398]Ibn kimweri.
Ramadhani Juma Kimweri
0746328046.

Mashairi mengine soma Shairi: Hakuna siri tena
 
Back
Top Bottom