Shairi: Nyege ni kunyegezana by Andanenga



Ufafanuzi wa nyege ni kunyegezana katika Kiswahili
nyege ni kunyegezana | Ufafanuzi katika Kiswahili - Oxford Living Dictionaries



    • nyege ni kunyegezana
MSEMO
1wema ni mpaka uwe wa kutendeana.


Maana yake, wema wa kufanywa upande mmoja tu, si wema, ni unyonyaji na utumwa.

Kwa kweli "Nyege ni kunyegezana" ni msemo wa Kiswahili uliokuwepo miaka mingi kabla Amiri Akida "Sauti ya Kiza" Andanenga hajaandika shairi la jina hilo.Maana yake, gwiji wetu Andanenga hakujizushia tu kuandika shairi hilo, bila muongozo, alilitoa katika misemo ya Kiswahili.

Halafu msemo wa "Nyege ni kunyegezana" ni msemo mrefu sana, hata neno lenyewe "nyege" limekuwa over sexualized.Kwa tunaojua Kiswahili cha ndani, nyege ni tamaa fulani hivi, si lazima hata iwe ya sex.Yani ni hamu kubwa, mtu kusema "nina nyege na movie ya action leo" ni kitu cha kumaanisha nina hamu ya kuangalia movie ya action, nothing sexual.

Kwahiyo huo msemo wa "Nyege ni kunyegezana" ulivyokuwepo zama na zama, unaweza kuwa mpana sana, kumaanisha.

Kimsingi, msemo unasisitiza reciprocity and propagation

1. Habari ni kupashana
2. Mapenzi ni kupendana
3. Kazi ni kushirikiana
4. Familia ni kuzaliana
5.Shughuli ni kukaribishana
6. Chakula ni kugawana
7.Heshima ni kuheshimiana
9. Uzuri ni kukubaliana
10. Vicoba ni kukopeshana
 

Ni kweli. Na hata kwenye kamusi upo na upo tokea zamani tu.

Kamusi zote za Kiswahili nilizonazo huo msemo upo!!
 
Heshima yako mkuu Kiranga , hakika kiswali unakijua vema.Asante kwa ufafanuzi mzuri na mifano uloyomaliza nayo hapo mwisho.
 

11. Kula ni kulana
 
Na mimi nasema kwetu Nyegezi na nyege ni kunyegezana.
 
Oh, wameufungia? Wengine tunaucheza on repeat in retaliation.

 
Tunaendeshwa na kick

BASATA wana overreact sana.

Badala ya kuweka utaratibu maalumu [kama vile PG-13 au Parental Advisory: Explicit Lyrics], wao wanakimbilia kufungia fungia tu.

Nachukiaga sana wanapozifungia nyimbo za wasanii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…