Shairi: Sina kosa

Shairi: Sina kosa

ramadhani kimweri

Senior Member
Joined
Apr 22, 2016
Posts
181
Reaction score
179
Sina wivu na wewe, kwani huyu ni mkeo
Ananifwata mwenyewe, toka kale sio leo
Natamani uelewe, kisha uwe na upeo
Mkeo kaanza kwangu, na mimi ndio wa mwanzo.

Mimi sinayo makosa, japo siyatendi mema
Mkeo yanamtesa, ni yale mambo ya zama
Nilifungua kitasa, kovu bado la muuma
Dawa yake ipo kwangu, hicho hasa ndio chanzo.

Wataka nifanye nini, akija nimkimbie
Mwaka sasa ishirini, bado aniwaza mie
Mimi ninakosa gani, wala usinichukie
Anakumbuka ya tangu, zama zile za michezo.

Mkeo anakupenda, na tena anakujali
Lakini anakidonda, Dawa yake si asali
Kajaribu kumkanda, uumpe njema kauli
Anachokifwata kwangu, ni kumpoza mawazo.

Sisi tunapokutana, twakumbuka ya zamani
Kucheka kutaniana, anakuwa na amani
Lakini kikubwa sana, wewe humpi thamani
Ndio mana huja kwangu, kulitafuta tulizo..

[emoji2398]Ibn kimweri.
Ramadhani Juma kimweri.
0746328046.

Mashairi mengine soma Shairi: Hakuna siri tena
 
Sina wivu na wewe, kwani huyu ni mkeo
Ananifwata mwenyewe, toka kale sio leo
Natamani uelewe, kisha uwe na upeo
Mkeo kaanza kwangu, na mimi ndio wa mwanzo.

Mimi sinayo makosa, japo siyatendi mema
Mkeo yanamtesa, ni yale mambo ya zama
Nilifungua kitasa, kovu bado la muuma
Dawa yake ipo kwangu, hicho hasa ndio chanzo.

Wataka nifanye nini, akija nimkimbie
Mwaka sasa ishirini, bado aniwaza mie
Mimi ninakosa gani, wala usinichukie
Anakumbuka ya tangu, zama zile za michezo.

Mkeo anakupenda, na tena anakujali
Lakini anakidonda, Dawa yake si asali
Kajaribu kumkanda, uumpe njema kauli
Anachokifwata kwangu, ni kumpoza mawazo.

Sisi tunapokutana, twakumbuka ya zamani
Kucheka kutaniana, anakuwa na amani
Lakini kikubwa sana, wewe humpi thamani
Ndio mana huja kwangu, kulitafuta tulizo..

[emoji2398]Ibn kimweri.
Ramadhani Juma kimweri.
0746328046.

Mashairi mengine soma Shairi: Hakuna siri tena

Hatari Kubwa!

Nimekumbuka utunzi, akiimba Marijani
Nilikuwa si mjuzi, kuuelewa kichwani
Akimkanya mzinzi, mke wa wake jirani!
Aliimba Marijani, sawa kucheza na moto!

Sawa kucheza na moto, na miye nafikiria
Kukumbuka ya utoto, wakati unavizia?
Utapata mkong'oto, huruma nakuonea
Aliimba Marijani, kasema hatari kubwa!

Kaimba hatari kubwa, vya watu ukivizia
Umeshakuwa mkubwa, kichwani ninashangaa
Huogepei kubambwa? wakati wadokolea?
Aliimba Marijani, unachezea hatari!

Waichezea hatari, na tena unapotea
Wajisifia mahiri, wakati unavizia?
Na mimi hapo nakiri, hatari waichezea
Aliimba Marijani, na tena kasisitiza

Tano nasema kikomo, ujumbe namalizia
Naomba upate somo, uwache vya kuvizia
Uliwache hilo shimo, kwa siri waangamia
Aliimba Marijani, sawa kuzcheza na moto!!

Nduguyo,

Choveki.
 
Sina wivu na wewe, kwani huyu ni mkeo
Ananifwata mwenyewe, toka kale sio leo
Natamani uelewe, kisha uwe na upeo
Mkeo kaanza kwangu, na mimi ndio wa mwanzo.

Mimi sinayo makosa, japo siyatendi mema
Mkeo yanamtesa, ni yale mambo ya zama
Nilifungua kitasa, kovu bado la muuma
Dawa yake ipo kwangu, hicho hasa ndio chanzo.

Wataka nifanye nini, akija nimkimbie
Mwaka sasa ishirini, bado aniwaza mie
Mimi ninakosa gani, wala usinichukie
Anakumbuka ya tangu, zama zile za michezo.

Mkeo anakupenda, na tena anakujali
Lakini anakidonda, Dawa yake si asali
Kajaribu kumkanda, uumpe njema kauli
Anachokifwata kwangu, ni kumpoza mawazo.

Sisi tunapokutana, twakumbuka ya zamani
Kucheka kutaniana, anakuwa na amani
Lakini kikubwa sana, wewe humpi thamani
Ndio mana huja kwangu, kulitafuta tulizo..

[emoji2398]Ibn kimweri.
Ramadhani Juma kimweri.
0746328046.

Mashairi mengine soma Shairi: Hakuna siri tena
Mke wa mtu ni sumu, wahenga wasisitiza
Unatutambia humu, mapenzi unayaweza
Haukumwona muhimu, we ukamtelekeza
Penzilo halikudumu, ngoma ulishindwa cheza

Sasa wajifanya fundi, wanawake kuwalea
Tukuweke lipi kundi, mjuaji wajitia
Siagi toka mtindi, nyuma watakupakia
Tuone nani mshindi, kadhia wajitakia

Ulishindwa mpa tunzo, limfaalo mrembo
Wapaswa kupata funzo, lilokushinda kitambo
Ulipaswa hapo mwanzo, kumshawishi kwa nyimbo
Upendo muhimu nyenzo, kisha charaza na'yo mbo

Mwanamke ana hila, Adam alimtenda
Akitaka hizo hela, hashindwi kugawa tunda
Juu chini atalala, uamini akupenda
Atakwachia msala, kwa mwingine ataenda

Mpe heshima mwenzio, achana na mke wake
Ni uanaume huo, kwanini urushwe teke?
Usipende Umario, kwa wanaume Temeke
Jitazame kwa kioo, una tabia za kike
 
Back
Top Bottom