ramadhani kimweri
Senior Member
- Apr 22, 2016
- 181
- 179
Sina wivu na wewe, kwani huyu ni mkeo
Ananifwata mwenyewe, toka kale sio leo
Natamani uelewe, kisha uwe na upeo
Mkeo kaanza kwangu, na mimi ndio wa mwanzo.
Mimi sinayo makosa, japo siyatendi mema
Mkeo yanamtesa, ni yale mambo ya zama
Nilifungua kitasa, kovu bado la muuma
Dawa yake ipo kwangu, hicho hasa ndio chanzo.
Wataka nifanye nini, akija nimkimbie
Mwaka sasa ishirini, bado aniwaza mie
Mimi ninakosa gani, wala usinichukie
Anakumbuka ya tangu, zama zile za michezo.
Mkeo anakupenda, na tena anakujali
Lakini anakidonda, Dawa yake si asali
Kajaribu kumkanda, uumpe njema kauli
Anachokifwata kwangu, ni kumpoza mawazo.
Sisi tunapokutana, twakumbuka ya zamani
Kucheka kutaniana, anakuwa na amani
Lakini kikubwa sana, wewe humpi thamani
Ndio mana huja kwangu, kulitafuta tulizo..
[emoji2398]Ibn kimweri.
Ramadhani Juma kimweri.
0746328046.
Mashairi mengine soma Shairi: Hakuna siri tena
Ananifwata mwenyewe, toka kale sio leo
Natamani uelewe, kisha uwe na upeo
Mkeo kaanza kwangu, na mimi ndio wa mwanzo.
Mimi sinayo makosa, japo siyatendi mema
Mkeo yanamtesa, ni yale mambo ya zama
Nilifungua kitasa, kovu bado la muuma
Dawa yake ipo kwangu, hicho hasa ndio chanzo.
Wataka nifanye nini, akija nimkimbie
Mwaka sasa ishirini, bado aniwaza mie
Mimi ninakosa gani, wala usinichukie
Anakumbuka ya tangu, zama zile za michezo.
Mkeo anakupenda, na tena anakujali
Lakini anakidonda, Dawa yake si asali
Kajaribu kumkanda, uumpe njema kauli
Anachokifwata kwangu, ni kumpoza mawazo.
Sisi tunapokutana, twakumbuka ya zamani
Kucheka kutaniana, anakuwa na amani
Lakini kikubwa sana, wewe humpi thamani
Ndio mana huja kwangu, kulitafuta tulizo..
[emoji2398]Ibn kimweri.
Ramadhani Juma kimweri.
0746328046.
Mashairi mengine soma Shairi: Hakuna siri tena