Shaka alisema Jumapili ya leo kuna jambo zito Rais Samia atalifanya. Ni jambo gani hilo? Au alitudanganya?

Shaka alisema Jumapili ya leo kuna jambo zito Rais Samia atalifanya. Ni jambo gani hilo? Au alitudanganya?

Katibu mwenezi wa CCM Taifa ndugu Shaka A. Shaka na siku chache baadaye mwanamama Ditopile waliutangazia umma kuwa Jumapili hii tutege macho na masikio Ikulu, maana Mhe Rais atakuja na jambo zito Sana

Mimi nasubiria bila kuchoka, natamani mhe Rais amalize haraka shughuli anayoifanya pale Dodoma ya kuzindua Mpango wa kupambana Uviko-19 ili aende kwenye tukio tuliloahidiwa na Shaka pamoja na Ditopile

Nitasikitika Sana kama Shaka na mwenzake Ditopile watakuwa waliuhadaa umma kwa jambo lisilokuwepo. Hii itakuwa ni kuibagaza taasisi ya Urais na Rais mwenyewe.
Tangu walipotunga na kutuimbia ule wimbo wa "CCM ni ileile" sijawahi kutegemea jipya kutoka CCM na watu wake
 
Ambao utarudi kwa wananchi kwa 100%.

Anza kujipanga na tenda za cement na vifaa vya ujenzi kama una hardware, kama ww ni mkandarasi kamata tenda yako, kama ww ni fundi anza kutafuta connection kwa wakandarasi kama ni mama ntilie anza kutafuta chimbo la kuhudumia vibarua.

Ukipata pesa nenda kalipe wafanyakazi wa ndani, boresha gesti house yako uajiri zaidi, fungua kabiashara uajiri hata watu wawili n.k nchi inaenda kuchangamka.

Kama ww ni mwanasiasa wa upinzani endelea kuponda.
Wewe endelea kuvaa kibwaya ili upongeze na kutukuza kwa nguvu zote wakati nyumbani kwenu huna uhakika wa milo mitatu huna.
 
Tangu walipotunga na kutuimbia ule wimbo wa "CCM ni ileile" sijawahi kutegemea jipya kutoka CCM na watu wake
John Komba alikuwa anajua kuwafanyia fix mboga mboga
 
Wewe endelea kuvaa kibwaya ili upongeze na kutukuza kwa nguvu zote wakati nyumbani kwenu huna uhakika wa milo mitatu huna.
🤣🤣🤣🤣🤣
Wacha we. Wewe jibu lako ni jepesi tu. Una Makisio sana. Maisha ya makisio ni tabu tupu.
 
Wacha wewe kujibaraguza
Una makisio yasiyo na uhalisia.

Una miezi tisa ya kujiposition kua sehemu ya mkopo utakaolipwa na sisi wananchi, achana na mm kukisia kisia usiyoyaelewa, angalia fursa kama unaziitaji.
 
Hujasikia kwa mh.Rais akitoa hotuba ya mrejesho wa Urais wake kwa miezi 6 iliyopita na atakachofanya kwa miezi 6 ijayo?

Una matatizo ulijia jambo zito ni kulipua makombora kama ya Kim?

Miezi 6 ajira rasmi 29,900 ..nani aliajiri kama mama?

Shirika la nyumba litaanza upya kumalizia mradi wa Kawe uliokufa,regency na morroco..

Wastaafu wamelipwa mafao sh.1.45 Tilioni nk

Kubwa.zaidi miezi 6 ijayo hakuna kupeleka madawati shule wala kuchangishana michango pesa ipo,sekta ya Afya ndio kabisaa vituo vya afya 150 vinajengwa na vingine vingi vitaanza baada ya kuzindua mpango wa leo..

Ni hivi kiufupi amefauli pakubwa imagine uwekezaji wa Til 5 miradi zaidi ya 3,000 vitatoa ajira rasmi zaidi ya 42,000 ..Hapo vipi?

Nani kama Samia? Samia hoyeee
SawaMOKOJANI
 
Una makisio yasiyo na uhalisia.

Una miezi tisa ya kujiposition kua sehemu ya mkopo utakaolipwa na sisi wananchi, achana na mm kukisia kisia usiyoyaelewa, angalia fursa kama unaziitaji.
Over my dead body
 
Katibu mwenezi wa CCM Taifa ndugu Shaka A. Shaka na siku chache baadaye mwanamama Ditopile waliutangazia umma kuwa Jumapili hii tutege macho na masikio Ikulu, maana Mhe Rais atakuja na jambo zito Sana

Mimi nasubiria bila kuchoka, natamani mhe Rais amalize haraka shughuli anayoifanya pale Dodoma ya kuzindua Mpango wa kupambana Uviko-19 ili aende kwenye tukio tuliloahidiwa na Shaka pamoja na Ditopile

Nitasikitika Sana kama Shaka na mwenzake Ditopile watakuwa waliuhadaa umma kwa jambo lisilokuwepo. Hii itakuwa ni kuibagaza taasisi ya Urais na Rais mwenyewe.

Shaka ni msemaji wa Rais toka lini? Yeye ni msemaji wa mwenyekiti wa CCM na si Rais wa nchi unless kuna vitu vimenipita.
 
Mkuu mbona unaheshima kubwa sana hapa jamvini?

Tangu lini Shaka akawa na jambo lililotimilika?
Tayari bi, Chokochoko ametoa lake la rohoni , kwamba yeye anaweza mitala yake tu ya Makunduchi haya ya kuongoza nchi ni makubwa kwake na yamemshinda.
 
Back
Top Bottom