Shaka aongoza operesheni maalum kilomita 15 kuwaondoa wafugaji wavamizi Kilosa

MTANZANIA620

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
105
Reaction score
116
DC SHAKA AONGOZA OPERESHENI PORI KWA PORI ENEO LA MKADAGE

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, ameongoza operesheni kubwa ya kukamata wafugaji wavamizi kwa kutembea kwa miguu zaidi ya kilomita 15 pori kwa pori, milimani na kwenye mito, akiambatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya.

Operesheni hiyo imefanyika katika eneo la Mkadage, ambako wafugaji wavamizi walikuwa wamejificha kwenye mabonde, milima na vichaka, wakiingiza mifugo yao kulisha na kuharibu mazao ya wakulima.

Katika operesheni hiyo, vikosi vya usalama vimefanikiwa kukamata wafugaji wavamizi pamoja na mifugo yao, na kubomoa vibanda vya kujifichia vilivyojengwa kiholela katika eneo hilo.

Hatua hiyo imeonyesha dhamira thabiti ya uongozi wa wilaya kusimama na wananchi na kuhakikisha sheria inafuatwa bila upendeleo ili kuleta ustawi na amani kwa wananchi wote.

Hata hivyo, DC Shaka amesisitiza kuwa msimamo wa serikali ni kuwa operesheni itaendelea katika eneo lote la Mkadage na maeneo mengine, hadi wafugaji wote wavamizi watakapoondoka, na wale watakaobainika kuhusika watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
---
 
Uongo mtupu, huyu shaka ndio kinara wa kuwatetea wafugaji hapo Kilosa, maeneo ya kata ya Magomeni kuanzia Mkadage, Masimba, Masugu, Tende, bonde la Kisaki mpaka Manzoka kote huko wafugaji wamasai wanalisha kwenye mashamba ya wakulima na yeye ndiye mtetezi namba moja. Tunajua amepewa kundi la ng'ombe zaidi ya elfu 1 na hao wafugaji kama rushwa amelipeleka Kongwa ranchi. Katika wakuu wa wilaya wa hovyo huyo ni mmojawapo sema analindwa kwa kuwa ni mtu wa karibu na Samia.
 
Picha iko wapi ?.
 
Waanze na Viongozi wa Vijiji husika na Hawa Wanasiasa Madiwani.. Kisha Viongozi wa Polisi na Polisi Jamii kwenye hayo maeneo..

Hawa ndiyo hupokea Rushwa na kuwalinda Hawa Wafugaji wasiokuwa na ustaarabu..
 
Uongo mtupu, huyu shaka ndio kinara wa kuwatetea wafugaji hapo Kilosa, maeneo ya kata ya Magomeni kuanzia Mkadage, Masimba, Masugu, Tende, bonde la Kisaki mpaka Manzoka kote huko wafugaji wamasai wanalisha kwenye mashamba ya wakulima na yeye ndiye mtetezi namba moja. Tunajua amepewa kundi la ng'ombe zaidi ya elfu 1 na hao wafugaji kama rushwa amelipeleka Kongwa ranchi. Katika wakuu wa wilaya wa hovyo huyo ni mmojawapo sema analindwa kwa kuwa ni mtu wa karibu na Samia.
Kumbe na yeye ana hizi tuhuma?
 
Back
Top Bottom