Shaka: Ni marufuku kwa hospitali za Serikali kumtoza Mama mjamzito kiasi chochote cha fedha wakati, kabla na baada ya kujifungua

Hu

Huyo ndio msemaji wa CCm Taifa chama kilichounda serikali na kuikabidhi serikali ili isimamie ilani, Sasa wewe puuza maagizo yake Ndio utajuwa Ni nani
Kwani wameanza kusema hivo leo?

Au leo ndio limekua agizo jipya?πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kama mke wako atadaiwa mpigie ndio utajua yeye ni nani?
Na wewe umeingizwa mkenge?

TOZO za miamala ni kubwa kuliko Tozo za uzazi.

Achana na wanasiasa , fanya yako mwenyewe. Na huyo ni msemaji tu wa chama , atasema chochote
 
Nitachangia bila kuweka porojo za siasa. Hii sera utekelezaji wake ni mgumu sana.

Kundi la wajawazito, watoto chini ya umri wa miaka 5 na wazee ndilo linalohudhuria zaidi katika vituo vya huduma za afya na ndilo linapaswa kupewa msamaha kwa mujibu wa sera.

Hii hupelekea mzigo mkubwa wa gharama za uendeshaji kwa vituo hivi, na kuingia kwenye madeni (umeme, maji, dawa, taka nk).

Ushauri wangu:
1. Ujauzito sio dharula, wazazi wa mtoto wana muda wa miezi 9 kujipanga hivyo wachangie gharama kidogo za huduma isipokuwa kwa huduma za dharula.

2. Kila mtanzania awe na Bima ya Afya, itungwe sheria ya kuwezesha utekelezaji wa hili.

Mwisho: "Afya ni ghali, na hakuna matibabu ya bure, ukiona umepatiwa huduma bila malipo jua kuna mtu/taasisi/nk imetoa gharama kwa ajili yako."
 

Aache utapeli wa kijinga, hiyo porojo inapigwa kila siku na bado wa mama wanatozwa pesa.
 
Mkuu uko sahihi 1000%

Ujauzito si dharula.

Ukiacha hata miezi 9 ya kusubiri kujifungua, kupata mimba tu huwa ni mipango. Kama uko kwenye reproductive age, na unafanya ngono zembe, huwezi sema umepata mimba kwa bahati mbaya. Unakuwa umejipanga 100%.

Tusifanye siasa kwenye mambo ya msingi.
 
Hivi kwani tatizo ni kutozwa tozo au huduma?

Mwambie zile Hospitali wanazotumia wao waheshimiwa wetu kuna sio tozo tu bali ni mitozo tena waifuata wenyewe hiyo mitozo.

Hivyo badala ya kurudia chorus zile zile miaka nenda rudi nendeni huo Hospitalu muhakikishe tunapata huduma kama mnazopata kule mnapozifuata tozo za hiari.
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘
Safi sana! Ila tutakoma zile nyodo za manesi
 
Hii itachangia watu kuzidi kuzaa kwa kasi,ilitakiwa watu wawezeshwe kiuchumi wachague hospital wanazotaka kwenda.
 
Ukiwa hujawahi kuitumikia serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania unaweza kuamini hiyo tozo itaondolewa. Wewe uliyeandika Rudi Bukene baadaye uje utwambie kama hawatozwi. Shaka aliwaambia wananchi wa Bukene wanachotoka kukisikia na wakashangalia. Waulize watumishi walitaka kusikia mshahara umepanda walichoambulia hakijulikani. Matamko kama haya yanawapa watumishi wa umma ugumu wa kufanya kazi zao. Serikali imeweka hizo tozo na si daktari Wala nesi na hazifutwi kwa kusherehesha kama Shaka anavyofanya.
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘
Safi sana! Ila tutakoma zile nyodo za manesi
Na upo hapo unaamini tozo zimefutwa. Pata ujauzito kajifungulie Bukene mahali tamko lilipotolewa halafu uje useme kama tozo zimefutwa. Bahati mbaya kubwa ni kuamini matamko ya wanasisa
 
Rais Samia ni jembe kwelikweli,tumuunge mkono
 
Rais Samia Suluhu anaupendo sana aliahidi kupunguza vifo vya mama na mtoto na ametimiza na sasa watatibiwa bure hili ni jambo jema sana
 
Huyu mjomba ni jembe kwelikweli
 
Mbona maneno hayo yapo miaka mingi na hatekelezeki. Alishindwa MAGU ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…