Shaka, tukusikilize wewe na CCM au Serikali?

Shaka, tukusikilize wewe na CCM au Serikali?

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Kauli ya Shaka kutengua amri ya mkuu wa mkoa inaonesha umuhimu wa ulazima wa katiba mpya, serikali za nchi zenye mfumo wa vyama vingi serikali ndiyo huongoza nchi na wananchi tunatakiwa tuisikilize serikali na si vinginevyo.

Bahati mbaya hivi sasa CCM imejipa jeuri ya kuidharau serikali na kutuaminisha sisi kuwa CCM ndiyo yenye amri zote nchini!

Kitendo cha CCM kinaondoa uhalali wa serikali kuwepo jambo ambalo halina afya kwa taifa.

Pia soma:

Thread 'Shaka apiga ‘stop’ agizo la kuzuia bodaboda, bajaji kuingia katikati ya Mji wa Dar' Shaka apiga ‘stop’ agizo la kuzuia bodaboda, bajaji kuingia katikati ya Mji wa Dar
 
Kauli ya Shaka kutengua amri ya mkuu wa mkoa inaonesha umuhimu wa ulazima wa katiba mpya, serikali za nchi zenye mfumo wa vyama vingi serikali ndiyo huongoza nchi na wananchi tunatakiwa tuisikilize serikali na si vinginevyo. Bahati mbaya hivi sasa CCM imejipa jeuri ya kuidhsrsu serikali na kutuaminisha sisi kuwa CCM ndiyo yenye amri zote nchini! Kitendo cha CCM kinaondoa uhalali wa serikali kuwepo jambo ambalo halina afya kwa taifa.

Hiyo tabia iliota mizizi enzi ya jiwe acha iendelee tu
 
Shaka anatuonesha nchi inaendeshwa holela, yaani mwanaccm anayejiona ana nguvu ya sauti hata akina Masudi Kipanya basi anajitokeza hadharani na kukemea.
 

Attachments

  • 2969395_hechejohn_20211017_1.mp4
    1.9 MB
Maccm hayakupewa kura bali yalipora uchaguzi kupitia polisiccm na Tume FEKI ya uchaguzi.

Kwa kuwa unaamini hivyo, kwamba Maccm hayakupewa kura bali yalipora uchaguzi, basi amini pia kuwa Maccm yanawajibika kuhakikisha Serikali yao inatimiza ahadi zake kwa Wananchi ili wahalalishe "wizi" huo.

Kimsingi Chama cha siasa, chochote duniani, huwajibika kusimamia utekelezaji wa Ilani yake ya Uchaguzi (ahadi kwa wapiga kura) kupitia Serikali iliyoiunda
 
Back
Top Bottom