CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,621
- 5,029
MANENO MANENO YASIKUKATISHENI TAMAA, RAIS SAMIA SULUHU HASSAN YUKO IMARA SANA
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema Rais Samia Suluhu Hassan yuko imara, makini na aliyetayari kuwatumikia Watanzania.
Shaka ameyasema hayo leo Novemba 5, 2022, jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi katika kongamano la kumpongeza Rais Samia kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya kuwatumikia na kuwaletea maendeleo wananchi, lililoandaliwa na Jukwaa la Jamii Mpya na kufanyika katika ukumbi wa PTA Temeke.
"Upo msemo unaosema mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe, niwahakikishie Rais Samia Suluhu Hassan yuko makini, yuko imara na amejawa na utayari wa kuwatumikia Watanzania, manenomaneno yasiwakatishe tamaa, manenomaneno yasiwarudishe nyuma kwa Rais wenu, hakuna kurudi nyuma Rais Samia Suluhu Hassan amesimama imara," amesema.
Mwisho